Nenda kwa yaliyomo

Yuda Barsaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yuda Barsaba alikuwa nabii (Mdo 15:32) na Mkristo maarufu wa Yerusalemu katika karne ya 1.

Kadiri ya kitabu cha Matendo ya Mitume (katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo) Mtaguso wa Yerusalemu (50 hivi) ulipomalizika, alitumwa pamoja na Sila huko Antiokia ili waongozane na Mtume Paulo na Barnaba na kuwatangazia Wakristo wa huko maamuzi ya mtaguso (Mdo 15:22)[1].

  1. Douglas, J D; Tenney, Merrill, whr. (1 Oktoba 1987), "Barsabbas", New International Bible Dictionary, Grand Rapids: Zondervan, uk. 126, ISBN 978-0-310-33190-2, iliwekwa mnamo 13 Januari 2013{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yuda Barsaba kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.