Yosefu wa Arimataya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yosefu wa Arimataya alivyochorwa na Pietro Perugino.
Yosefu akimuomba Pilato ruhusa ya kumzika Yesu, kadiri ya James Tissot.

Yosefu wa Arimataya alikuwa Myahudi mwanamume wa karne ya 1, maarufu hasa kutokana na habari zake zinazopatikana katika Injili (Mk 15:42-46; Math 27:57-60; Lk 23:50-53; Yoh 19;38-42).

Habari za ziada, lakini si za kuaminika, zinapatikana katika vitabu ambavyo havimo katika Biblia ya Kikristo, hasa Injili ya Nikodemu.

Tajiri na mtu wa baraza la Israeli, aliyetarajia Ufalme wa Mungu uliotangazwa na Yesu, alichukua jukumu la kumzika, akiomba ruhusa ya Ponsyo Pilato na kujitolea kaburi alilokuwa amejiandalia pangoni kwenye Kalivari[1].

Anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na madhehebu mengine ya Ukristo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Agosti[2] au nyingine.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yosefu wa Arimataya kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.