Nenda kwa yaliyomo

Yoramu wa Israeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Yoramu alivyochorwa mwaka 1553.

Yoramu wa Israeli (kwa Kiebrania יְהוֹרָם, Yəhorām; 868 KK hivi - 841 KK hivi) alikuwa mwana wa mfalme Ahabu na malkia Yezebeli akatawala kwa miaka 12 Ufalme wa Israeli baada ya kaka yake Ahazia aliyefariki bila kuacha watoto.

Biblia inamhukumu hasa kwa kuendeleza sera ya kidini iliyoanzishwa na Yeroboamu I ikiwataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi, ingawa hakufuata sana sera ya wazazi wake ya kutaka Waisraeli waabudu Baali badala ya YHWH.

Aliuawa na Yehu ambaye alijifanya mfalme badala yake na kurudisha Israeli kwa Mungu pekee kama alivyoagizwa na nabii Elisha.

Habari za Yoramu zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme, 3-9.

    Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
    Je, unajua kitu kuhusu Yoramu wa Israeli kama habari za maisha au kazi yake?
    Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
    Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.