Yondo Sister

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yondo Sister
Jina la kuzaliwaYondo Kusala Denise
AmezaliwaZaire, Kongo ya Kibelgiji sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kazi yakeMwimbaji, mwanamuziki
AlaSauti
Miaka ya kazi1980–hadi sasa
StudioAir B. Mas Production, Melodie, T.J.R. Music

Yondo Kusala Denise (amezaliwa tar. 1 Januari 1958) ambaye anajulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Yondo Sister, ni msanii wa Kikongo. Wengi humwita "malkia wa soukous", "Tina Turner" wa muziki wa dansi barani Afrika. Yondo Sister amepata kuwa mwimbaji mkuu katika bendi ya Soukous Stars kwa miaka kadhaa kabla ya kwenda kufanyakazi kama msanii wa kujitegemea. Uwezo wake wa kuimba iliibuliwa na Lutu Mabangu wakati huo Yondo akiwa kama mnenguahi wa Tabu Ley katika bendi yake ya Rocherettes. Yondo muziki uko katika damu, mzee wake alikuwa akipiga muziki kwa kujifurahisha tu, humo kukajengeka ujasiri wa kutoogopa hadhira. Na mara kadhaa alishiriki katika dansi, polepole na kuja kuwa mwanamuziki kamili na kutoa albamu ya kwanza mwaka 1991.[1]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya diskografia ya albamu za Yondo Sister.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]