Yohane wa Montecorvino
Yohane wa Montecorvino (Montecorvino Rovella, Campania, Italia, 1247 – Beijing, China. 1328) alikuwa Mfransisko wa Italia aliyepata umaarufu kutokana na safari zake za kimisionari barani Asia.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kufanya umisionari Ulaya Mashariki, alitumwa kwa Papa kama balozi wa Patriarki wa Konstantinopoli. Baadaye alitumwa na Papa kuinjilisha Wamongolia wa Persia.
Kutoka huko alikwenda Chennai, India kwa miezi 13, na hatimaye Beijing, China (1294). Huko, akiwa peke yake kwa miaka 11, aliweza kujenga kanisa la kwanza mwaka 1299 na la pili mwaka 1305.
Kutokana na mafanikio hayo, mwaka 1307 Papa Klementi V alimtumia Wafransisko wenzake saba waliofanywa maaskofu ili waende kumfanya askofu mkuu. Kati yao watatu tu walifika na kutimiza agizo hilo (1308).
Kwa miaka 20 iliyofuata aliyendelea kueneza Kanisa Katoliki sehemu mbalimbali za China. Baada ya kifo chake, Kanisa hilo lilidumu miaka 40.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Sir Henry Yule (ed.) Cathay and the Way Thither, London: Hakluyt Society, 1914, Vol. III, pp. 45-58. Contains two letters by Montecorvino.
- Jackson, Peter (2005). The Mongols and the West: 1221-1410. Longman. ISBN 978-0-582-36896-5.
- This article incorporates text from the 1913 Catholic Encyclopedia article "John of Montecorvino" by Otto Hartig, a publication now in the public domain.
- The manuscripts of Montecorvino's Letters exist in the Laurentian Library, Florence (for the Indian Epistle) and in the National Library, Paris, 5006 Lat.-viz. the Liber de aetatibus, fols. 170, v.-172, r. (for the Chinese). They are printed in Wadding, Annales minorum (A.D. 1305 and 1306) vi. 69-72, 91-92 (ed. of 1733, &c.), and in the Münchner gelehrte Anzeigen (1855), No. 22, part in. pp. 171175. English translations, with valuable comments, are in Sir H. Yule's Cathay, i. 197-221.
- See also Wadding, Annales, v. 195-198, 199-203, vi. 93, &c., 147, &c., 176, &c., 467, &c.; C. R. Beazley, Dawn of Modern Geography, iii. 162-178, 206-210; Sir H. Yule, Cathay, i. 165-173. (C. R. B.)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Medieval Sourcebook: John of Monte Corvino: Report from China 1305 Archived 14 Agosti 2014 at the Wayback Machine..
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |