Yohane Plessington

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yohane Plessington (Garstang, Lancashire, Uingereza, 1637 hivi – Tyburn, London, Uingereza, 19 Julai 1679) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki kuanzia 25 Machi 1662 alipopata upadirisho huko Segovia (Hispania).

Kisha kurudi Uingereza, alifanya utume wake kwa siri, kutokana na dhuluma ya serikali.

Hatimaye alikamatwa na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kueneza imani Katoliki. Hivyo alinyongwa na kuraruliwa chini ya mfalme Charles II[1].

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 23 Mei 1920, halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini[2].

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.