Yohane Mbatizaji wa Rossi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Yohane Mbatizaji wa Rossi (Voltaggio, Piemonte, 22 Februari 1698Roma, 23 Mei 1764) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Italia.

Papa Pius IX alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Mei 1860, halafu Papa Leo XIII akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Desemba 1881[1].

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa maskini, alikwenda Roma kwa masomo[2] akapewa upadrisho ingawa aliugua kifafa.

Tangu hapo alijitosa kuhudumia wanawake fukara pamoja na wagonjwa, wafungwa, wafanyakazi na hasa kuadhimisha sakramenti ya upatanisho kwa wengi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]