Nenda kwa yaliyomo

Yocheved Bat-Miriam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yocheved Bat-Miriam (; jina la kalamu la Yocheved Zhlezniak) (5 Machi 1901 – 7 Januari 1980) alikuwa mshairi kutoka nchi ya Israeli. Bat-Miriam alizaliwa nchini Belorussia (kwa sasa Belarus) katika familia ya Mayahudi wa Kihasidi. Alisomea ualimu (pedagogy) mjini Kharkov na katika vyuo vikuu vya Odessa na Moscow. Katika kipindi hiki, alishiriki katika harakati za fasihi za kimapinduzi za kikundi cha "Hebrew Octoberists", ambacho kilikuwa kikundi cha fasihi cha Kikomunisti, na mfululizo wa mashairi yake ya mapema, yaliyokuwa wimbo wa sifa kwa Urusi ya kimapinduzi yenye kichwa cha habari Erez (Nchi), ulichapishwa kwenye antholojia ya kikundi hicho mnamo mwaka 1926.[1] Ni wa kipekee miongoni mwa washairi wa lugha ya Kiebrania kwa kuonyesha hamu na kumbukumbu za mapenzi (nostalgia) kwa mandhari ya nchi aliyozaliwa. Yocheved alihamia Palestina ya Kiingereza (ambayo baadaye ilikuja kuwa Israeli) mnamo mwaka 1928.[2] Kitabu chake cha kwanza ya ushairi, Merahok ("Kutoka mbali") kilichapishwa mnamo mwaka 1929. Mnamo mwaka 1948, mtoto wake wa kiume, Nahum (Zuzik) Hazaz, aliyemzaa na mwandishi Haim Hazaz, alifariki katika Vita vya Palestina vya 1947–1949. Tangu wakati huo, hakuwahi kuandika shairi lingine tena.

Moshe Lifshits, Israel Zmora, mwenyeji Luba Goldberg, Avraham Shlonsky, Lea Goldberg, na Yocheved Bat-Miriam (mwaka 1938)
  1. Zierler, Wendy. "Yokheved Bat Miriam (Zhelezhniak)". Jewish Women's Archive.
  2. Ben Gurion University of the Negev. Yocheved Bat-Miriam – Curriculum Vitae Archived Julai 27, 2011, at the Wayback Machine
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yocheved Bat-Miriam kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.