Yewande Akinse
Yewande Akinse (alizaliwa kama Yewande Adebowale, Lagos, Nigeria, tarehe 25 Septemba 1992) ni mshairi, mwandishi na mjasiriamali kutoka Nigeria. Yeye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni za Salubata, PAP.earth na Plychain.
Ametunukiwa tuzo ya African Adaptation Solutions Challenge pamoja na Tuzo ya Vijana wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Youth Award) kuhusiana na mkutano wa 2022 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Kigali, Rwanda.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Yewande Akinse alisoma katika Shule ya St. Mary’s Private School, Ajele, Lagos kabla ya kuendelea na masomo ya sekondari katika Holy Child College, Lagos.
Alipata Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B) na Shahada ya Uzamili ya Sheria (LL.M) katika Chuo Kikuu cha Lagos. Mwaka 2014 alipata pia cheti cha B.L kutoka Nigerian Law School.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Akinse ni mwanasheria, mjasiriamali wa kijamii, mshairi na mwandishi, pamoja na mtetezi wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi. Ni mwanzilishi mwenza wa PAP.EARTH, injini ya utafutaji inayolenga kupunguza hewa ya ukaa (CO₂) na kudhibiti mabadiliko ya tabianchi, pamoja na Salubata, kampuni inayotengeneza viatu vinavyoweza kubadilishwa (modular shoes) kwa kutumia taka za plastiki zilizorejelewa.
Ameshachapisha mashairi zaidi ya 110. Miongoni mwa kazi zake ni mkusanyiko wa mashairi A Tale of Being, of Green and of Ing (2019) na Voices: A Collection of Poems that Tell Stories (2016).
Mwaka 2021, Akinse alikuwa miongoni mwa wajasiriamali vijana 15 wa Afrika waliotunukiwa tuzo ya kwanza ya African Youth Adaptation (YouthADAPT) Solutions Challenge. Mwaka 2022, Rais wa zamani wa Nigeria, Muhammadu Buhari, alimpongeza kwa kuwa miongoni mwa washindi wanne bora katika shindano la Vijana wa Jumuiya ya Madola wakati wa mkutano wa CHOGM uliofanyika Kigali, Rwanda. Tarehe 8 Septemba 2022, alishinda tuzo ya World Bank YouthActOnEDU Spoken Word.
Vitabu
[hariri | hariri chanzo]- Voices: A Collection of Poems that Tell Stories (2016)
- A Tale of Being, of Green and of Ing (2019)
Tuzo na heshima
[hariri | hariri chanzo]- Tory Burch Entrepreneur Fellow (2024)
- African Adaptation Solutions Challenge
- Commonwealth Youth Green Guru Award
- Tuzo ya Fidelity Bank ya Uandishi Bunifu (2013)
- Tuzo ya Gazeti la The Guardian (TGN) kwa Ushairi (2019)
- Project Knucklehead Prize for Creative Rebellion (2020)
- World Bank YouthActOnEDU Spoken Word Prize (2022)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yewande Akinse kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |