Nenda kwa yaliyomo

Yerusalemu ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Yerusalemu ya Mashariki (kijani); pamoja na makazi mapya ya Israeli katika eneo la Palestina (buluu nyeusi)

Yerusalemu ya Mashariki ni ile sehemu ya mji wa Yerusalemu iliyotawaliwa na Yordani kati ya 1948 na 1967 halafu kutwaliwa na Israel wakati wa vita ya siku sita ya 1967. Sehemu hii ni pamoja na "mji wa kale" na mahali patakatifu pa dini tatu za Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Baada ya vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948 Yerusalemu iligawiwa kwa pande mbili:

  • Yerusalemu ya Magharibi au "mji mpya" ikawa upande wa Israel
  • Yerusalemu ya Mashariki au "mji wa kale" ikawa upande wa Yordani.

Wayahudi waliokaa upande wa mashariki (mtaa wa Kiyahudi katika mji wa Daudi) walipaswa kuondoka, vivyo hivyo wakazi Waarabu waliokaa upande wa magharibi.

Mji ulikua sana upande wa Israel ukawa mji mkuu wa nchi. Sehemu ya mashariki haikuona maendeleo makubwa kama mji mmojawapo wa Yordani.

Baada ya vita ya 1967 Israeli iliingiza sehemu ya mashariki katika manisipaa yake ya Yerusalemu ya Israel, kwa jumla 6.4 km² ya Yerusalemu ya Yordani na 64 km² za vijiji vya eneo la magharibi ya Yordani. Wakazi wa mji wa mashariki hawakuulizwa na jumuiya ya kimataifa haikubali hatua hiyo.

Mamlaka ya Palestina inatumaini ya kwamba siku moja sehemu ya mashariki ya Yerusalemu itakuwa mji mkuu wa Palestina. Israel inasimama imara ya kwamba mji hutagawiwa tena.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Yerusalemu ya Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.