Yemen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yemen


Yemen (Kiarabu: الجمهورية اليمنية ) ni nchi kusini mwa Bara Arabu.

Imepakana na Omani, Saudia na Bahari Hindi.

Nchi za karibu ng'ambo ya mlango wa bahari wa Bab el Mandeb ni Eritrea, Jibuti na Somalia.

Eneo lake ni pamoja na kisiwa cha Sokotra na visiwa 200 vingine.

Historia

Hadi mwaka 1990 palikuwa na nchi mbili za Yemen ya Kaskazini na Yemen ya Kusini zilizoungana tarehe 22 Mei 1990.

Ile ya kaskazini ilikuwa Ufalme wa Yemen baada ya Imamu Yahya Muhamad wa kundi la Zaidiya kuvamia velayat ya Yemen ya milki ya Waturuki Waosmani (1 Novemba 1918). Baadaye ikawa Jamhuri kwa njia ya mapinduzi (1962).

Ile ya kusini ilikuwa sehemu koloni (Aden) na sehemu nchi lindwa (Hadramaut) ya Waingereza. Baada ya ukoloni kwisha ikawa mara moja Jamhuri (30 Novemba 1967).

Watu

Wakazi wengi ni Waarabu wa makabila mbalimbali; wengine ni machotara wa Kiarabu-Kiafrika, Waajemi na Wazungu.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarabu.

Upande wa dini, wananchi karibu wote (99%) ni Waislamu, wakiwemo Wasuni (60–65%) na Washia (35-40%). Waliobaki ni Wakristo, Wayahudi, Wahindu au hawana dini yote.

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Yemen bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Yemen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.