Yehoyada

Yehoyada (kwa Kiebrania: יְהוֹיָדָע, Yəhōyāḏā‘, "YHWH anajua"; aliishi karne ya 9 KK) alikuwa kuhani wa hekalu la Yerusalemu na mume wa Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa mwandamizi wake Ahazia[1].
Huyo alipofariki dunia kwa kuuawa bado kijana, mama yake, Atalia binti Ahabu, aliteka madaraka kwa kuua watoto wa Ahazia na kuendeleza sera za ufalme wa Israeli dhidi ya Mungu pekee, YHWH.
Hata hivyo, Yehosheba alifaulu kumuokoa mtoto wa mwaka mmoja, Yehoashi, akamlea kwa siri hekaluni akishirikiana na Yehoyada, hata wakaweza kumtawaza katika kiti cha enzi cha babu yao Daudi[2][3].
Baadaye Yeyohada alijitahidi sana kurudisha Israeli kwa Mungu wake pekee.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 11 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 22-24.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hammer, Jill (2022-11-30). "The Problem of Jehosheba: Reading One Biblical Character in Two Different Feminist Ways by Jill Hammer". Feminism and Religion (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-06-21.
- ↑ Barnes, W. E. (1899),Cambridge Bible for Schools and Colleges on 2 Chronicles 23
- ↑ Laffey, Alice L (1998). An Introduction to the Old Testament: A Feminist Perspective. Fortress Press. uk. 139. ISBN 978-0800620783.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Bench, Clayton H. The Coup of Jehoiada and the Fall of Athaliah: The Discourses and Textual Production of 2 Kings 11. Piscataway: Gorgias Press, 2016.
| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yehoyada kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |