Nenda kwa yaliyomo

Yehoramu wa Yuda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Yehoramu alivyochorwa na Guillaume Rouillé mwaka 1553.

Yehoramu wa Yuda (kwa Kiebrania: יְהֹורָם, Yəhōrām, yaani Yahweh ametukuka; pia: יוֹרָם Yōrām; 882 KK hivi - 842 KK hivi) alitawala ufalme wa Yuda kati ya miaka 849 KK na 842 KK baada ya kuua ndugu zake 6.

Kwa kuoa Atalia, binti Ahabu, alifuata sera za ufalme wa Israeli dhidi ya Mungu pekee, YHWH, kinyume na alivyofanya baba yake Yehoshafati. Biblia inaeleza ndiyo sababu ya kushindwa kutawala kwa mafanikio.

Aliyemrithi ni mwanae Ahazia.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 8 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 21-22.

Pia anatajwa na Injili ya Mathayo kati ya mababu wa Yesu Kristo.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  • McFall, Leslie (1991), "Translation Guide to the Chronological Data in Kings and Chronicles" (PDF), Bibliotheca Sacra, 148: 3–45, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2010-08-27
  • Tetley, M. Christine (2005). The Reconstructed Chronology of the Divided Kingdom (tol. la illustrated). Eisenbrauns. ISBN 978-1575060729.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yehoramu wa Yuda kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.