Nenda kwa yaliyomo

Yehoashi wa Israeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Yehoashi alivyochorwa mwaka 1553.

Yehoashi wa Israeli (kwa Kiebrania יְהוֹאָשׁ, Yəhō’āš) alikuwa mwana wa Yehoahazi na mjukuu wa mfalme Yehu akatawala kwa miaka 16 Ufalme wa Israeli (798 KK hivi - 782 KK hivi[1]).

Biblia inamhukumu hasa kwa kuendeleza sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi[2]. Hata hivyo alimheshimu nabii Elisha[3].

Kadiri ya utabiri wake, Yehoashi alishinda Syria na kuteka miji yake kadhaa. Muda mfupi kabla hajafa, alimshinda pia mfalme Amazia wa Yuda [4][5].

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme, 13-14.

  1. Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257
  2. "Joash, Jehoash;" New Bible Dictionary. Douglas, J.D., ed. 1982 (second edition). Tyndale House Publishers, Wheaton, IL, USA. ISBN 0-8423-4667-8, pp. 597–598
  3. Adam Clarke's Commentary on the Holy Bible. Clarke, Adam. 1967. Beacon Hill Press, Kansas City, KS, USA. pp. 372–373
  4. 2 Kings 14:9–10; "Joash var. Jehoash." The Anchor Bible Dictionary, Vol III, 1992. Freedman, David Noel., ed., New York: Doubleday. ISBN 0-385-19361-0 pp. 857–858
  5. 2 Kings 13:13; "Joash, Jehoash." Illustrated Dictionary & Concordance of the Bible. Wigoder, Geoffrey, ed., 1986. G.G. The Jerusalem Publishing House Ltd. ISBN 0-89577-407-0
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yehoashi wa Israeli kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.