Yasmin Mrabet
Mandhari

Yasmin-Katie M'rabet (kwa Kiarabu: ياسمين-كاتي مرابط; alizaliwa 8 Agosti 1999) ni mchezaji wa soka wa kitaalamu anayekipiga kama kiungo wa katikati kwa klabu ya Valencia. Alizaliwa nchini Hispania, lakini hucheza kama beki wa kati katika timu ya taifa ya wanawake ya Morocco. Kabla ya kuwakilisha Morocco, aliwakilisha taifa la kuzaliwa kwake katika ngazi ya vijana chini ya miaka 19.
M'rabet alizaliwa mjini Madrid kwa baba Mmoroko na mama Mwingereza. Anazungumza lugha za Kihispania, Kiingereza, Kifaransa, na Kikatala kikamilifu.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "YASMIN: Yasmin Katie Mrabet Slack". Txapeldunak (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yasmin Mrabet kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |