Yasinto wa Krakau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Yasinto akitokewa na Bikira Maria

Yasinto wa Krakau, O.P. (kwa Kipolandi: Jacek Odrowąż; 1185 - 15 Agosti 1257) alikuwa padri wa Polandi ambaye alipokutana na Dominiko wa Guzman huko Bologna (Italia) alijiunga na shirika lake jipya.

Baadaye alitumwa kulieneza katika Ulaya Mashariki (Polandi na Ukraina)[1].

Papa Klementi VIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1594.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Agosti[2], lakini pia 17 Agosti.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/66250
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Innocenzo Cybo Ghisi, Vita e miracoli di san Giacinto confessore dell'Ordine de predicatori, Verona, 1594
  • Marcantonio Baldi, Della vita, miracoli, & canonizatione di San Giacinto Pollaco dell'ordine di San Domenico, Venezia, 1594
  • Marie Agoult de Flavigny, San Giacinto e I suoi tempi: VII centenario della morte, 1257- 1957, Roma, 1957
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.