Nenda kwa yaliyomo

Yash Ghai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yash Pal Ghai (amezaliwa 20 Oktoba 1938) ni msomi wa Kenya katika sheria ya katiba. Kufikia mwaka 2007 alikuwa mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Katiba cha Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa nchini Nepal. Hadi mwaka 2008, alikuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kambodia kuhusu haki za binadamu. Mnamo Septemba 2008, alijiuzulu wadhifa wake kufuatia mabishano makali na Serikali ya Kambodia.[1] Amechaguliwa kuwa Mwanachama wa British Academy tangu mwaka 2005. Yash Pal Ghai ni mwandishi na mshairi. Maandiko yake yanayojulikana yamejikita zaidi katika mjadala wa sheria ya katiba barani Afrika.

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Babu zake walitoka katika familia ya Khukhrain ya Khatri, waliotoka katika mkoa wa Punjab wa Kaskazini mwa India, na walikuwa sehemu ya wimbi la wakimbizi wa Kihindi katika katika Afrika Mashariki, uliokuwa ukiungwa mkono na Milki ya Kiengereza. Baba yake alimpeleka Ghai katika Chuo Kikuu cha Oxford kusoma.[2][2][3]

  1. 1 2 "Professor Yash Ghai C.V." (PDF). University of Hong Kong. Iliwekwa mnamo 31 Machi 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Scholarly Exchange and Visitors - University of Wisconsin Law School".
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yash Ghai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.