Yared wa Ethiopia
Mandhari
Yared wa Ethiopia (kwa Kige'ez: ቅዱስ ያሬድ; 25 Aprili 505 - 20 Mei 571[1][2]) ni kati ya Wakristo maarufu wa Ethiopia[3].
Aliishi katika Ufalme wa Axum katika karne ya 6. Anatajwa kama mtunzi na mwanzilishi wa muziki wa Kikristo nchini, muziki wa utamaduni wa Ethiopia na wa Eritrea. Alikuza muziki wa kidini wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia, na matumizi katika muziki wa liturujia, pamoja na mfumo wa nota wa Ethiopia. Zaidi ya hayo, alitunga Zema, au mapokeo ya nyimbo za Ethiopia-Eritrea, ambazo zinaimbwa hadi leo.[4]
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Mei.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Chavis, Charles L. (2011-04-05). "Yared (Saint), 505-571 AD" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-05-03.
- ↑ Giday, Belai (1991). Ethiopian Civilization (kwa Kiingereza). B. Giday.
- ↑ https://dacb.org/stories/ethiopia/yared/
- ↑ "Saint Yared (505-571) •" (kwa American English). 2011-04-05. Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- A brief History of Saint Yared Archived 10 Desemba 2016 at the Wayback Machine.
- Biography of Saint Yared Archived 28 Julai 2011 at the Wayback Machine.
- Charles L. Chavis Jr. Saint Yared
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |