Yannick Bolasie
| Taarifa binafsi | |||
|---|---|---|---|
| Tarehe ya kuzaliwa | 24 Mei 1989 | ||
| Mahali pa kuzaliwa | Lyon, France, | ||
| Kimo | 1.88 m | ||
| Nafasi anayocheza | Winga | ||
Yannick Bolasie (alizaliwa 24 Mei 1989) ni mchezaji wa mpira wa miguu ambaye hucheza kama winga katika klabu ya Chapecoense, inayoshiriki Campeonato Brasileiro Série A.
Amecheza katika mfumo wa ligi za mpira wa miguu nchini England akiwa na klabu za Plymouth Argyle, Barnet, Bristol City, Crystal Palace, Everton, Aston Villa, Middlesbrough na Swansea City.
Alizaliwa nchini Ufaransa na kukulia nchini England. Aliichezea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mechi 50 kati ya mwaka 2013 na 2022.
Historia ya klabu
[hariri | hariri chanzo]
Mwanzo wa maisha ya soka
[hariri | hariri chanzo]Bolasie alianza maisha yake ya soka akiwa na umri wa miaka 16 katika klabu ya Rushden & Diamonds. Alikaa kwa muda wa miezi minne katika timu yao ya vijana, kisha akacheza kwa kipindi fulani katika klabu ya Hillingdon Borough, iliyokuwa ikishiriki Southern Football League, kabla ya kuhamia barani Ulaya kucheza katika klabu ya Floriana, iliyokuwa ikishiriki Maltese Premier League.
Historia ya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Bolasie alikuwa na sifa za kuiwakilisha kimataifa Ufaransa, England na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutokana na mahali alipozaliwa, alikokulia na asili yake.
Mwezi Januari 2013, wakati akicheza katika Championship akiwa na Crystal Palace, Bolasie alikataa nafasi ya kuiwakilisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Kombe la Mataifa ya Afrika 2013, akisema kwamba hakutaka kuvuruga maendeleo ya maisha yake ya soka katika ngazi ya klabu.
Mwezi Machi 2013, Bolasie aliitwa tena katika kikosi cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.na akacheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2014, ambapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilitoka sare ya 0–0 dhidi ya Libya.
Bolasie alichaguliwa katika kikosi cha Kongo kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2015 lililofanyika nchini Equatorial Guinea. Alifunga bao la kusawazisha katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi, uliomalizika kwa sare ya 1–1 dhidi ya Zambia katika uwanja wa Estadio de Ebibeyin tarehe 18 Januari. Timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya tatu.
Heshima
[hariri | hariri chanzo]Crystal Palace
- Mchujo wa kupandishwa daraja wa Football League Championship: 2013
- Mshindi wa pili wa Kombe la FA: 2015–16
Binafsi
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.soccerbase.com/players/player.sd?player_id=50619
- ↑ https://www.premierleague.com/en/players/55452/yannick-bolasie/overview
- ↑ https://www.bbc.com/sport/football/47073854
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yannick Bolasie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |