Nenda kwa yaliyomo

Yaa Ntiamoah Baidu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yaa Ntiamoa-Baidu

Chair MiDA
Rais Nana Akuffo-Addo

mhitimu wa University of Ghana
taaluma Academic
Fani yake Zoologist

Yaa Ntiamoa Baidu ni mtaalamu wa wanyama wa Ghana, ana utaalamu juu ya mazingira, ana usomi na taaluma wa usimamizi. Kwenye tarehe Machi 2017, alichaguliwa kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Milenia ya Ghana. Alifanya kazi kwa nafasi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ghana mpaka ilivyofika wakati wake wa kustaafu mnamo wa 2011. Yeye ni mwanakikundi wa Chama Kipya cha Uzalendo cha Ghana. [1]

Biografia

[hariri | hariri chanzo]

Ntiamoa-Badiu alipata elimu yake kwenye Shule ya Sekondari ya St. Monica kwa kiwango cha O level, kisha katika Shule ya Upili ya Konongo Odumase kwa kiwango cha A level. [2] Alisoma masomo ya chuoni kwenye Chuo Kikuu cha Ghana, mahali alipata shahada ya daraja la kwanza juu ya Zoolojia mwaka 1975, [2] kisha Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Edinburgh mwaka 1980. [2] Alifanikiwa kuwa mhadhiri kwenye Idara ya Zoolojia ya Chuo Kikuu cha Ghana, mwaka 1985, kisha profesa msaidizi kwa mwaka wa 1995. Mnamo 2003, alichaguliwa kama profesa kamili. [2] [3]

Alichaguliwa kujiunga na kamati ya usimamizi ya chuo kikuu kwa nafasi ya Makamu Mkuu wa Utafiti, Ubunifu na Maendeleo. Alivyokuwepo chuo kikuu, alishika nafasi ya mkurugenzi wa Kituo cha Ardhi Oevu za Afrika [4] na Chuo Kikuu cha Ghana Carnegie Kizazi Kijacho cha Wasomi bara la Afrika. [5] Alifanya kazi na Kwesi Yankah, ambaye alikuwa Makamu Mkuu wa Masuala ya Kielimu na Wanafunzi. Alikuwa mfanyakazi katika nafasi hiyo mpaka mnamo wa Julai 2011 alipostaafu kutoka chuo kikuu na wadhifa wake huo ukachukuliwa na Prof. John Gyapong. Mwaka 2005, Yaa Ntiamoa-Baidu alichaguliwa pamoja na maprofesa wengine wanne wa taaluma tofauti za kitaaluma kama wanafunzi wa Chuo cha Sanaa na Sayansi cha Ghana . [6]

Mwenyekiti wa Bodi ya MiDA

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa Machi 2017, Rais Nana Akufo-Addo alimchaguwa kushika nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya wanachama kumi na wanne ya Mamlaka ya Maendeleo ya Milenia. [7] Aliapishwa pamoja na wajumbe wengine wa bodi kwenye tarehe 13 Machi 2017 ndani ya Jumba la Flagstaff . Rais alimpa jukumu la kusimamia shughuli za bodi ili kufanikisha kwamba lengo lenyewe la makubaliano ya Pili ya Mkataba kati ya Serikali ya Ghana na Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani linafikiwa na kwa wakati sahihi. Kusudi lake kuu ni kutumia kwa hekima uwekezaji wa dola milioni 498.2 kutoka Shirika la Changamoto za Milenia ili kuweka ubora kwenye uzalishaji na usambazaji wa umeme kwa watu binafsi na makampuni. [7] [8] Mkataba huo una kipindi miaka mitano ambapo vipengele vyote vya makubaliano lazima vifanikishwe. [7]

  1. "Yaa Ntiamoah Baidu, Biography". mobile ghanaweb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-11-16. Iliwekwa mnamo 2023-11-16.
  2. 1 2 3 4 "Prof. Yaa Ntiamoa-Baidu Receives Award At The 3rd Ghana Women Of Excellence Award Ceremony". University of Ghana. 10 Machi 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link).
  3. "Middle-Income status requires entrepreneurial devt – Osagyefo". ghanaweb. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-01-11.
  4. "University of Ghana receives grant for Climate Change and Food Systems Research | University of Ghana". University of Ghana. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-04. Iliwekwa mnamo 2017-12-02.
  5. "Social reintegration of offenders and recidivism in Ghana" (PDF).
  6. "Middle-Income status requires entrepreneurial devt – Osagyefo". ghanaweb. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-01-11."Middle-Income status requires entrepreneurial devt – Osagyefo". ghanaweb. Retrieved 2018-01-11.
  7. 1 2 3 "President Akufo-Addo Swears In MiDA Board". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-03. Iliwekwa mnamo 2017-12-02.
  8. "Ensure clear road map on ECG concession – Nana Addo to MiDA board | Comprehensive Ghana Oil and Gas news, information, updates, analysis". reportingoilandgas. (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-05-18. Iliwekwa mnamo 2017-12-02.