Benedictus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wimbo wa Zakaria)
Zakaria akiandika jina la kumpa mtoto wake siku ya kumtahiri (sehemu ya mchoro wa Domenico Ghirlandaio, karne ya 15, Kikanisa cha Tornabuoni, Italia).
Maneno ya wimbo ulivyo katika Injili (kwa Kigiriki) kwenye Kanisa la Mt. Yohane Mbatizaji Mlimani, Ein Karem, kijiji anakosadikika kuwa alizaliwa.
Wimbo katika tafsiri ya Kiebrania.
Wimbo katika tafsiri ya Kiarabu.
Wimbo katika tafsiri ya Kilatini.

Benedictus ni neno la Kilatini lenye maana ya "Asifiwe". Ni maarufu kama jina la wimbo wa Kiinjili unaotumika kila siku katika Masifu ya asubuhi ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo.

Jina hilo linatokana na kwamba ndilo neno la kwanza katika tafsiri ya Kilatini ya wimbo huo ambao, kadiri ya Lk 1:68-79, Zakaria aliutunga siku ya kumtahiri ya mtoto wake, Yohane Mbatizaji. Katika nafasi hiyo alifungua tena kinywa chake na kutoa unabii.

Kabla ya hapo, kwa zaidi ya miezi tisa Zakaria alikuwa bubu na kiziwi kama adhabu ya kutosadiki mara maneno ya Malaika Gabrieli aliyetumwa na Mungu kumpasha habari ya kwamba sala zake na za mke wake Elisabeti zimekubalika, hivyo watazaa mtoto wa kiume, ingawa wote wawili ni wakongwe na Elisabeti ni tasa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benedictus kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.