Nenda kwa yaliyomo

Willie Kimani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Willie Kimani
Amezaliwa (1984-04-21)21 Aprili 1984
Amekufa 23 Juni 2016 (umri 32)
Amezikwa Kabete, Kiambu
Kazi yake mwanasheria wa haki za binadamu
Mwajiri Misheni ya Kimataifa ya Haki (IJM)
Mwenza Hannah Wanjiku Gitwiria
Watoto 2
Wazazi Paul Kinuthia (Baba) Elizabeth Wambui (Mama)

Willie Kimani Kinuthia (21 Aprili 1984 – 23 Juni 2016) alikuwa mwanasheria wa haki za binadamu nchini Kenya aliyeuliwa akitekeleza wajibu wake kazini. Tukio hilo ni mojawapo ya kesi kubwa zaidi za ukatili na unyanyasaji wa polisi nchini Kenya.[1] Willie Kimani alikuwa akifanya kazi na Misheni ya Kimataifa ya Haki (IJM) katika mji mkuu wa Nairobi. Vilevile, alikuwa mwanachama wa bodi ya Ulinzi wa Kuendeleza Haki na pia mwanachama wa Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK).[2]

Kabla ya kifo chake, Willie alikuwa amehusika na kesi dhidi ya afisa wa polisi Fredrick Leliman. Kesi hii iliwasilisha awali kortini na Josephat Mwenda aliyekuwa mwendeshaji wa pikipiki. Hii ilifuatia tukio lililotendeka mnamo Aprili 2015, wakati ambapo afisa Leliman alidaiwa kumfyatulia risasi Josephat Mwenda mkononi bila kuchokozwa wala sababu na kisha kumshtaki kwa makosa kadhaa ya kubuni na yaliyo uwongo katika juhudi za kuficha ufyatuaji risasi.[3] Kutokana na unyanyasaji huo ulioendelea kwa muda, Josephat aliwasilisha malalamishi kwa Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA). Ilipofika mwezi wa Disemba 2015, Josephat alishtakiwa tena kwa makosa sita mapya ya trafiki, ikiwa ni pamoja na kuendesha pikipiki yake bila kofia ya usalama. Misheni ya Kimataifa ya Haki (IJM) ilichukua kesi hiyo Februari 2016, na kumteua Willie kumwakilisha na kushughulikia kesi hiyo.[4]

Mauaji nje ya mfumo wa kisheria

[hariri | hariri chanzo]

Siku ya 23 Juni 2016, Kimani pamoja na Josephat Mwenda, na dereva wao wa teksi, Joseph Muiruri, walitekwa nyara kwa nguvu na maafisa wanne wa Polisi wa Utawala wa Kenya na baadaye kuuawa kinyume cha utaratibu wa sheria.[5][6] Tukio hili la utekaji bila mchakato wa kisheria lilijiri wakati ambapo watatu hao walikuwa wakiondoka mahakamani kule Mavoko baada ya kutajwa kwa kesi yao.[7]

Siku kadhaa baadaye, tarehe 1 Julai, miili yao ilipatikana Mto Ol-Donyo Sabuk, mikono yao ikiwa imefungwa nyuma ya migongo yao na miili yao ikiwa na alama za kuonyesha kuwa walikuwa wameteswa kabla ya kuuliwa.[2]

Kesi ya kisheria mahakamani

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya uchunguzi kufanywa kwa muda wa wiki tatu, maafisa wanne wa polisi wa kitengo cha utawala nchini: Fredrick Leliman, Stephen Cheburet, Silvia Wanjiku, na Leonard Mwangi walishtakiwa na kufikishwa mahakamani tarehe 18 Julai 2016 kwa makosa matatu ya kuteka nyara na uuliwaji wa Kimani, Mwenda na Muiruri.[8][9]

Tarehe 24 Juni 2021, familia yake Willie Kimani ilitoa wito wa kuharakishwa kwa kesi hii ambayo bado ilikuwa ikiendelea, miaka 5 baada ya mauaji yake.[10] Mnamo Septemba 20, 2021, hakimu wa Kenya aliamua kwamba washtakiwa wanne walikuwa na kesi ya kujibu.[11]

Tarehe 22 Julai 2022 ilipowadia, wale maafisa watatu wa polisi; Fredrick Leliman, Stephen Cheburet, na Sylvia Wanjiku na mtoa taarifa wa polisi Peter Ngugi walipatikana na hatia ya makosa matatu ya mauaji ya Kimani, mteja wake Josephat Mwenda na dereva Joseph Muiruri. Kwa upande mwingine, afisa Leonard Maina Mwangi aliachiliwa huru baada ya kutopatikana na hatia yote katika mashtaka yote matatu ya mauaji.[12][13]

Mahakama ilitoa hukumu kwa washtakiwa mnamo tarehe 3 Februari 2023 kama ifuatavyo; Fredrick ole Leliman, afisa wa polisi aliyetajwa kuwa ndiye mpangaji wa mauaji hayo ya kinyama alipewa adhabu la kuhukumiwa kifo, Stephen Cheburet Morogo alifungwa kwa muda wa miaka 30. Sylvia Wanjiku Wanjohi alihukumiwa miaka 24.[14][15][16] Mdokezi, wa polisi aliyekuwa Peter Ngugi Kamau alipokea kifungo cha miaka 20 gerezani.[17] Hukumu hizi zilitolewa na kusomwa na Jaji Jessie Lesiit.[18]

Familia ya Willie Kimani

[hariri | hariri chanzo]

Kimani alikuwa mtoto wa Paul Kinuthia na Elizabeth Wambui.[19] Katika uzima wake, Willie alimpenda na kumwoa Hannah Wanjiku na pamoja walijaliwa watoto wawili.[19][20]

Tuzo na utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kuthamini kazi yake na kutambua mchango wake, Kimani alitangazwa kuwa Mwanasheria Bora wa Mwaka wa 2016 na kutunukiwa pia tuzo ya heshima baada ya kifo chake kwa ujasiri wake aliouonyesha kwa kutetea wanyonge na waliodhulumiwa nchini Kenya.[21]

Mnamo mwaka wa 2017 Kimani alipewa heshima kuu ya Tuzo ya Haki za Binadamu ya Padre Anthony Kaiser na Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK). Hii ilikuwa ishara ya kutambua ari yake na uthabiti katika kulinda haki na utu wa waliotengwa na kunyanyaswa katika jamii.[22]

Rapa Julius Owino, maarufu kama Juliani, alitunga na kuimba wimbo, Machozi Ya Jana. Wimbo huu uliandikwa kama kumbukizi na heshima kwa marehemu Willie Kimani pamoja na waathiriwa wengine wa mauaji ya kinyume cha sheria.[23][24]

  1. ↑ Correspondent (2022-07-22). "3 Police Officers Guilty of Killing Lawyer Willie Kimani". The Kenya Forum (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-08-19.
  2. 1 2 Kenya, Amnesty (2017-06-23). "We Shine a Light for Kenya's Mavoko Three". Amnesty International Kenya (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-09. Iliwekwa mnamo 2021-08-09.
  3. ↑ "Lawyer Willie Kimani His Client And Taxi Drver Found Dead" (kwa American English). 2025-06-11. Iliwekwa mnamo 2025-08-16.
  4. ↑ "Willie Kimani murder: A timeline". Daily Nation (kwa Kiingereza). 2022-12-16. Iliwekwa mnamo 2025-08-16.
  5. ↑ "Alleged Police Abuse in Kenya Escalates 'Beyond What Anyone Thought'". Voice of America (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 9, 2021. Iliwekwa mnamo 2021-08-09.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. ↑ "Dispatches: Four Police Officers Charged With Triple-Murder in Kenya". Human Rights Watch (kwa Kiingereza). 2016-07-18. Iliwekwa mnamo 2021-08-09.
  7. ↑ "Kenyan lawyer Willie Kimani 'abducted by rogue police'", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2016-06-30, iliwekwa mnamo 2025-08-21
  8. ↑ "Willie Kimani was held in cell but cops made no entry in OB". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-09.
  9. ↑ "Willie Kimani: Kenyan police charged with murder", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2016-07-18, iliwekwa mnamo 2025-08-21
  10. ↑ "Justice delayed, justice denied? Family of lawyer Willie Kimani marks five years since his gruesome murder". Citizentv.co.ke (kwa American English). 24 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 2021-08-09.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. ↑ "Kenya judge: policemen must answer for killing of human rights lawyer". SWI swissinfo.ch (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-20. Iliwekwa mnamo 2021-09-20.
  12. ↑ "3 officers found guilty, one acquitted in Willie Kimani murder case".
  13. ↑ "Willie Kimani murder: Police officer Leliman, three co-accused found guilty".
  14. ↑ Willie Kimani: Kenya ex-policeman sentenced to death for lawyer's murder (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2023-02-03, iliwekwa mnamo 2025-08-31
  15. ↑ "Willie Kimani murder case: Fredrick Leliman handed death sentence as co-accused jailed for 30 and 24 years". Citizen Digital (kwa Kiingereza). 2023-02-03. Iliwekwa mnamo 2025-08-16.
  16. ↑ GROUP, NTV KENYA-NATION MEDIA. "NTV Kenya: Willie Kimani murder case: Officer Fredrick Leliman sentenced to death". NTV Kenya (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-08-16.
  17. ↑ "Kenyan policemen get sentences for murder of human rights lawyer". Al Jazeera (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-08-16.
  18. ↑ Malalo, Humphrey (2023-02-03), "Kenyan police handed heavy sentences for rights lawyer's murder", Reuters (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2025-08-21
  19. 1 2 "I'll die before I get justice for my son's death – Willie Kimani's dad". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-09.
  20. ↑ Odenyo, Akello. "No closure: Our son is still waiting for his father, says slain lawyer's widow". The Standard (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-09.
  21. ↑ "It is Willie! The Late Human Rights Lawyer Willie Kimani named 2016 Juristof the Year – ICJ Kenya" (kwa American English). 14 Desemba 2016. Iliwekwa mnamo 2021-08-09.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  22. ↑ "LSK News › LSK Awards Lady Justice Mumbi Ngugi, George Oraro, SC and the late Willie Kimani, Advocate". lsk.or.ke. Iliwekwa mnamo 2021-08-09.
  23. ↑ "[VIDEO] Juliani's new song shines spotlight on extrajudicial killings". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-08-16.
  24. ↑ "How Juliani uses music to fight for a better planet". Daily Nation (kwa Kiingereza). 2023-07-14. Iliwekwa mnamo 2025-08-23.