William Coxen
Sir William George Coxen, Baronet wa 1 (23 Machi 1867 – 7 Aprili 1946) alikuwa mfanyabiashara na mwanasiasa wa Uingereza.[1]
Coxen alizaliwa huko Southwark,[1] akiwa mtoto wa kwanza wa George Nickels Coxen na Fanny Luxton, wa Newington, London. Alipata elimu yake katika shule ya Ongar Grammar School huko Essex na katika chuo cha King's College London. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, alihudumu kama Afisa Amiri (Commanding Officer) wa Kikosi cha 4 cha London Volunteer Rifles. Baada ya vita, alikuwa Meya wa Holborn kati ya mwaka 1919 na 1920, Mwenyekiti wa Baraza la Pamoja la Viwanda (Joint Industrial Council) la Wilaya ya London kati ya mwaka 1920 na 1922, Alderman wa London, Sheriff wa Jiji la London kati ya mwaka 1928 na 1929, na Meya Mkuu wa London kati ya mwaka 1939 na 1940. Pia alikuwa Mshika Hazina wa Hospitali ya Kitaifa ya Kifalme ya Orthopaedic (Royal National Orthopaedic Hospital) na Mdhamini wa Chama cha Uuguzi cha Metropolitan (Metropolitan Nursing Association). Alitunukiwa cheo cha knighted mnamo mwaka 1929</ref> na kupewa taji la baronet, wa Seal katika Wilaya ya Kent, mnamo mwaka 1941.</ref>
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu William Coxen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |