Nenda kwa yaliyomo

Wilfrid wa Ripon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nakala ya Vita Sancti Wilfrithi (karne ya 11).

Wilfrid wa Ripon au wa York (tahajia asili: Wilfrith[1]; Northumbria, 633 hivi – Oundle, Northamptonshire, 709 hivi) alikuwa mmonaki Mbenedikto, halafu abati na hatimaye askofu wa York, Uingereza kwa miaka 45 kuanzia mwaka 664, ingawa alilazimika mara kadhaa kuacha jimbo lake hilo kwa wengine.

Alishiriki Sinodi ya Whitby na kwa bidii yake alichangia sana uenezi wa umonaki wa Kibenedikto na mapokeo yote ya Kanisa la Kilatini kati ya waamini wa Ukristo wa Kiselti.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki[2], Waorthodoksi[3] na Waanglikana kama mtakatifu[4].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Aprili[5] au 12 Oktoba.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Fraser From Caledonia to Pictland p. 47
  2. "About the Diocese" Roman Catholic Diocese of Middlesbrough
  3. Hutchinson-Hall Orthodox Saints p. 78
  4. http://www.santiebeati.it/dettaglio/50680
  5. Martyrologium Romanum

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 354-355
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 312-313

Marejeo ya lugha nyingine

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]