Wilfred B. Akasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wilfred Boniphace Akasi alizaliwa tarehe 23/12/1989 huko jijini Mwanza Wilaya ya [[Nyagamana] katika hospitali ya Bugando .

          ELIMU

Mwaka 1999 alianza elimu yake ya shule ya msingi katika shule ya msingi Kawekamo iliyoko Wilaya ya Kwimba. Ambapo alihitimu mwaka 2005.

Mwaka 2006 alichaguliwa kuanza masomo yake ya sekondari katika shule ya Sekondari ya Mwamashimba iliyoko wilaya ya Kwimba ambapo alihitimu vizuri mwaka 2009.

Baada ya kuhitimu Wilfred alionyesha uwezo mzuri sana darasani hivyo alichukuliwa na shirika na vijana la umoja wa kimataifa (YUNA) huko alipewa fursa ya kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo uandishi wa makala mbali mbali za vijana. Mwaka 2010 alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari Nsumba iliyoko jijini mwanza mkabala na chuo cha mtakatifu Agustino. Akiwa shuleni hapo bafo aliendelea na uandishi wa makala mbali mbali za vijana na Umoja wa mataifa.

Mwaka 2012 Wilfred alimaliza kidato cha Sita na kufaulu kwa daraja la kwanza hivyo alichaguliwa kujiunga na chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini akichukuwa Shahada ha Maendeleo ya Mipango ya Fedha na Uwekezaji( (Bachelor Degree in Development Finance and Investment Planning).

Akiwa chuoni hapo aliweza pata ajira ya muda katika mradi mkubwa wa utafiti uliokuwa ukiendeshwa na Professa Mallila huku akijikita zaidi katika uandiashi wa makala mbali mbali.

Mwaka 2015 baada ya kuhitimu alipata ajira katika ofisi ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania .

Kwa sasa Wilfred licha ya kuajiriwa na serikali ni mwandishi na mjasiliamali. Katika tasnia ya uandiashi amendika kitabu kinachoitwa CHOZI LA SUNDI Kinachoongelea mauaji ya vikongwe na Alibino katika jamii ya Afrika Kitabu kilichochukuwa matukio mengi halisi yaliyowahi kutokea katika jamii.

Mbali na hilo Wilfred ana miswada mbali mbali ya Riwaya iliyoko mbioni kukamilika. Hii ni pamoja na:

Nje na uandishi wa riwaya, Wilfred ni mwandishi nguli wa tafiti na miradi ya kibiashara na kijamii. Pia ni mshauri mwelekeji katika masuala ya uwekezaji na ujasiliamali.