Moshi (mji)
Jiji la Moshi | |
Lua error in Module:Location_map at line 510: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Tanzania" does not exist.Mahali pa mji wa Moshi katika Tanzania |
|
Majiranukta: Page Module:Coordinates/styles.css has no content.3°20′24″S 37°20′24″E / 3.34000°S 37.34000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Kilimanjaro |
Wilaya | Moshi Mjini |


Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.
Wakazi[hariri | hariri chanzo]
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, mji huu una wakazi wapatao 184,292 [1]. Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga wakifuatiwa na Wapare na makabila mengine yaliyohamia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kama Wasambaa, Warangi n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.
Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanaenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.
Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.
Hali ya Hewa[hariri | hariri chanzo]
Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na kipindi cha joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.
Utalii[hariri | hariri chanzo]
Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.
Elimu[hariri | hariri chanzo]
Mji wa Moshi una vyuo vikuu vitatu:
- MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperative and Business Studies) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro
- MWUCE (Mwenge University College Of Education) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT (St. Augustine University - Mwanza)
- KCMC Medical School chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini
- O.U.T(The Open University of Tanzania) ambacho ni tawi la chuo chenye jina hilohilo chenye makao yake makuu jijini Dar es salaam.--
Utawala[hariri | hariri chanzo]
Kiutawala mji wa Moshi ni wilaya ya Mkoa wa Kilimanjaro. Ndani yake kuna kata 15 ambazo ni Bondeni, Kaloleni, Karanga, Kiboroloni, Kiusa, Korongoni, Longuo, Majengo, Mawenzi, Mji Mpya, Msaranga, Njoro, Pasua, Rau na Kilimanjaro.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Boma Mbuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiboriloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Moshi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|
- Pages with script errors
- Pages with TemplateStyles errors
- All articles with dead external links
- Articles with dead external links from January 2021
- Articles with invalid date parameter in template
- Mbegu za jiografia ya Mkoa wa Kilimanjaro
- Miji ya Tanzania
- Mkoa wa Kilimanjaro
- Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro
- Wilaya ya Moshi Mjini