Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Wiki Loves Ramadan 2025

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wiki Loves Ramadan 2025

Wiki Loves Ramadan ni shindano la kila mwaka la kimataifa linalolenga kuhifadhi na kushiriki desturi na tamaduni mbalimbali zinazoshuhudiwa wakati wa mwezi wa Ramadhani. Toleo la mwaka 2025 litazingatia nchi 32, zikiwemo Algeria, Bangladesh, Indonesia, Misri, Nigeria, Marekani, na India, ili kunasa utajiri wa tamaduni, urithi wa Kiislamu, na wasifu wa watu mashuhuri katika Uislamu. Michango itatolewa kwa zaidi ya lugha 26 kwenye majukwaa kama Wikipedia, Wikibooks, na Wikivoyage. Kupitia matukio ya mtandaoni na vipindi vya mafunzo, WLR 2025 inalenga kushirikisha jamii mbalimbali, kukuza usambazaji wa maarifa na kuthamini tamaduni.

Shindano hili linatarajiwa kufanyika kuanzia Februari 25 hadi Aprili 15, 2025, kwa lengo la kuboresha uwakilishi wa tamaduni za Ramadhani na urithi wa Kiislamu kwenye majukwaa ya Wikimedia.

Kanuni

Miongozo ya Uundaji Maudhui
  • Hali Nzuri: Wahariri hawapaswi kuwa na marufuku yoyote ya tabia mbaya kwenye mradi wowote wa Wikimedia tangu tarehe ya kuanza kwa shindano au wakati wa kipindi cha shindano.
  • Hakuna Maingizo ya Awali: Wahariri hawapaswi kuwasilisha makala walizozifanyia kazi kabla ya tangazo la shindano hili. Hii inapaswa kuwa mchango mpya kwa Wikipedia.
  • Tamko la Mgongano wa Kimaslahi: Wahariri wenye viashiria vya mizozo ya maslahi lazima waonyeshe hilo kwenye ukurasa wa majadiliano wa usajili wao na kuepuka kuhariri makala yoyote yenye maslahi ya moja kwa moja.
  • Hakuna Kujitangaza: Wahariri hawawezi kushiriki ili kujitangaza wao wenyewe au miradi yao binafsi.
  • Kipaumbele cha Makala: Maingizo yanaweza kuwa makala mpya au maboresho makubwa kwa makala zilizopo. Hata hivyo, maingizo lazima yawe na mtazamo wa mada zinazohusiana moja kwa moja na Ramadan, tamaduni za Kiislamu, au watu, sehemu, au desturi zinazohusiana ambazo hazijafunikwa vizuri kwenye Wikipedia. Kipaumbele kinapewa kwa uundaji wa makala mpya zaidi.
  • Viwango vya Marejeleo: Habari zote lazima ziweze kuthibitishwa na zisaidiwe na nukuu kutoka kwa vyanzo vya kuaminika, vyanzo vya pili, kama ilivyoorodheshwa katika miongozo ya Wikipedia. Nukuu lazima ziwe zimeundwa kwa usahihi na kuwekwa mahali panapofaa.
  • Mtazamo Huru: Makala lazima zifuate mtazamo huru, kuwasilisha habari kwa haki na bila upendeleo. Maoni yoyote lazima yahusishwe na vyanzo vya kuaminika.
  • Kufuata Haki za Nakala: Yaliyomo yote lazima yafuatilie sera za haki za nakala za Wikimedia. Maandishi na media zinazotumika lazima ziwe za asili au zenye leseni chini ya leseni ya Creative Commons inayolingana au kuwa katika eneo la umma.
  • Undani na Urefu wa Makala: Maingizo lazima yawe na kina kikubwa, yakifunika mada kwa njia kamili. Makala zinapaswa kwenda zaidi ya ufafanuzi wa msingi na kutoa habari yenye maarifa na kina. Kima cha chini cha maneno 400 ya yaliyomo mapya yanayohitajika kwa makala mpya, na kima cha chini cha maneno 300 ya yaliyomo mapya yanayohitajika kwa makala iliyoboreshwa, maingizo lazima yaonyeshe kiwango cha kujitolea na kina ili kustahiki. Ubora, kina, utafiti na ufanisi ni muhimu zaidi kuliko urefu wa makala. Makala fupi hayatakubaliwa. Yaani, mstari mmoja.
  • Lugha na Kalima ya Ustaarabu: Makala lazima zifuate lugha na kalima inayofaa kwa Wikipedia, ikiwa ni pamoja na lugha rasmi na ya heshima na kuepuka maneno yoyote ya uchochezi au ya matusi. Makala pia yanapaswa kuwa rahisi kusomeka na kueleweka na msomaji wa kawaida.

Hakuna Tafsiri za Mashine: Matumizi ya tafsiri za mashine pekee hayakubaliki. Makala yote, iwe imetafsiriwa kikamilifu au la, lazima yakaguliwe na binadamu kuhakikisha kuwa ni ya kusomeka. Sio mkasi na gundi pekee.

Maelekezo ya Uwasilishaji

Maingizo yote lazima yameainishwa chini ya jamii iliyobainishwa wazi kwenye toleo la lugha husika la Wikipedia. Jamii hii itakuwa: <tvar name="1">Jamii:Michango ya Wiki Loves Ramadan 2025</tvar> (inapaswa kutafsiriwa kwa lugha yako ya ndani).

Maingizo yote lazima yawasilishwe kabla ya 15 Aprili 2025, saa 23:59 UTC.

Maingizo lazima yaunganishwe na shindano maalum na pia yanapaswa kujumuisha tag kwenye ukurasa wa majadiliano, ili yaweze kutambulika kwa urahisi kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Evaluation Criteria
  • 1 point should be given for a accepted article, and 0 will be for a rejected article. This will applicable for all submitted articles.
  • The Best Newcomer will be identified by local team of organisers and jury members. For more suggestion, please see the suggested additional judging criteria for best newcomer on Meta-Wiki.
  • To know more rules and criteria about this contest follow the link.

Sign up

Sign up and report your contributions in the tool. We suggest signing up on the event registration page as well!

Muandaaji

Waamuzi