Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala ya wiki/Ramadan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ramadan au ramadhani, (kwa Kiarabu: رمضان) ni mwezi wa tisa katika Kalenda ya Kiislamu na mwezi wa kufunga katika Uislamu kuadhimisha ufunuo wa kwanza wa Qur'an kutona na mafundisho ya Mtume Muhammad. Mwezi huo huwa na siku 29 au 30 kutegemeana na kuonekana kwa mwezi.

Kufunga ni moja ya Nguzo tano za Uislamu. Mwislamu mzima, mwenye afya nzuri, anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya kufunga chakula na kinywaji mchana kutwa, pamoja na kujizuia kufanya mapenzi toka alfajiri hadi magharibi.

Matendo hayo ya toba yanaendana na kuswali sana na kusoma Quran kwa wingi.

Kwa wagonjwa, wanaosafiri, wazee, wajawazito, wanaonyonyesha na wanawake wenye hedhi sio lazima kufunga.

Mwisho wa Ramadhani ni sikukuu ya Idul Fitri (عيد الفطر - ʿīdu ʾl-fiṭr) ambayo ni sherehe ya furaha na kupongezana. Waislamu hutoa zakat (zakatul-fitri زكاة الفطر) na kuswali, baadaye hukutana kwenye karamu.

Neno Ramadhani linatokana na mizizi ya Kiarabu ramiḍa au ar-ramaḍ, ambayo inamaanisha joto kali au ukavu. ►Soma zaidi