Wikipedia:Kiswahili Wikipedia Challenge/Submissions/Sj

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Katiba

Katiba ni mkusanyiko wa sheria kwa serikali mara nyingi huwa maandishi yanayoelezea-mamlaka na utendaji wa mfumo wa kisiasa. Katika mfumo wa nchi, neno hili linamaanisha katiba ya kitaifa inayofafanua misingi ya kanuni za kisiasa, na kuanzisha utaratibu, mamlaka na majukumu, ya serikali.Kwa kudhibiti majukumu na mamlaka ya serikali, katiba hudhamini baadhi ya haki za wananchi.Neno hili katiba linanaweza kutumika kwa ujumla kumaanisha sheria yoyote ambayo inafafanua utendaji wa serikali, ikiwa ni pamoja na katiba kadhaa za kihistoria zilizowahi kuwepo kabla ya maendeleo ya kisasa ya katiba za kitaifa.