Wikipedia:Kiswahili Wikipedia Challange/Submissions/nejwana wangu
|- | '''WALEMAVU NA MALENGO YA MILENIA NCHINI TANZANIA''' ||
UTANGULIZI
[hariri chanzo]MKUKUTA kwa lugha ya Kiswahili ni kifupi cha mpango wa Mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini, ambao ni chagizo katika malengo 8 Malengo ya Milenia. MKUKUTA ni zao la mashauriano na baraza la mawaziri na kuidhinishwa Februari 2005.
Walemavu kwa maana rahisi ni hali anayokuwa nayo mtu ambayo humzuia kutenda kama tu mwingine, ulemavu upo wa aina nyingi, wa kuzaliwa na wakusababishwa na vitu kama ajali na magonjwa. Kwa sasa, ulemavu wa kuzaliwa unakaribiana na ule wa ajali na magonjwa, pengine ni kutokana na kubadilika kwa hali ya mambo duniani. .
=Nini Maoni ya Walemavu=
Kuhakikisha kuwa mipango ya Serikali inatekelezwa kwa haki kwa makundi yote katika jamii, na kwa vyama vya Walemavu, pamoja na jukwaa la kawaida, na walemavu kushiriki katika mipango yenye manufaa kwa Taifa.
Hapa Tanzania kuna vyama 6 vikuu vya Watu wenye Ulemavu ambavyo ni wanachama wa SHIVYAWATA, muungano wa vyama vya Walemavu :
• Chama cha Wasioona Tanzania • Chama cha walemavu wa viungo Tanzania (CHAWATA) • Chama cha Maalbino Tanzania • Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) • Chama cha walemavu Akili • Chama cha Viziwi na Vipofu
Aidha kuna taasisi nyingine zinazoshughulika na masuala ya Ulemavu:
• Shirika la Maendeleo ya Kiuchumi na kijamii kwa Walemavu • Kituo cha Habari juu ya ulemavu. • Kituo cha Haki za Binadamu cha Watu wenye ulemavu 'S • Kikundi cha Watu wasiosikia na Maendeleo ya Kiuchumi (UMIVITA) • Taasisi ya Watu Wasioona Tanzania Idadi ya Walemavu nchini Tanzania kwa 2002 Kulingana na makadirio ya Shirika la Afya Duniani kuhusu ulemavu, mwaka 2002 Tanzania ilikuwa walemavu 3,456,900 '. amabapo idadi wananchi ilikuwa 34,569,232. Hawa wapo katika makundi yafuatayo: • Viwete kimwili, 967,932.= 28% • Vipofu 933,363, = 27% • Viziwi 691,380, = 20% • Ulemavu wa Akili 276,552, = 8% • Wenye utaahira 138,276, = 4% • Ulemavu mwingine 449,397, = 13%
Sensa ya watu iliyofanyika mwaka 2002, inaonyesha kuwa Tanzania ina Walemavu wengi zaidi kuliko inavyodhaniwa na kufikiriwa kuwa. Vyama vyote vya Walemavu vinajua ukweli kwamba wazazi huwaficha walemavu. Pia ni kweli kwamba idadi ya Walemavu hukua kwa sababu ya ajali, malaria, uti wa mgongo, utapiamlo na sababu nyingine.
MALENGO YA MILENIA
[hariri chanzo]Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini unalenga kushughulikia Malengo ya Milenia kwa: • Kutokomeza kabisa umaskini • Kutoa elimu ya msingi kwa wote • Kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake. • Kupunguza vifo vya watoto wachanga • Kutoa huduma bora ya afya ya uzazi • Kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine. • Kuhifadhi na kuweka mazingira endelevu. • Kukuza mshikamano miongoni mwa jamii ya kimataifa kwa ajili ya maendeleo.
Je malengo hayo ya milenia yana nafasi gain kwa Walemavu hapaTanzania? Walemavu wengi wamepokea kwa hisia mchanganyiko, kila mtu akija na jambo lake kama;
• wanaweza wasipate faida kwa sababu hawashirikishwi kikamilifu kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa na vyombo vya maamuzi. • Kwamba labda wao watafaidika kwa kiasi fulani, kwa sababu vyama vyao vilihojiwa na kuhusika katika hatua za upangaji.
Utekelezaji: Nini kimefanyika
[hariri chanzo]Serikali imeonyesha nia yake ya kushughulikia Malengo ya Milenia. Tumeona ongezeko kubwa katika shule za msingi nchini kote. Asilimia kubwa ya watoto wenye umri wa kwenda shule wamejiunga shule, idadi ya shule za sekondari imeongezeka. Kila kata sasa ina shule yake yenyewe.
Barabara zinajengwa na kuboreshwa, miundombinu ya maji imeboreshwa, huduma za afya zimeletwa karibu na watu, wanawake wanapewa nafasi sawa katika elimu na ajira. Walemavu je? Hali ya Walemavu bado ipo hatarini. Moja ya sababu ni kwamba katika sera ya Taifa, walemavu wamewekwa pamoja na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu; ambayo yanajumuisha: - wanawake, wajane, vijana, watoto, yatima na watu wanaoishi na VVU / UKIMWI.
Elimu ya Walemavu
[hariri chanzo]Serikali, kupitia mpango maalum wa elimu ya msingi umefikia ngazi ya kijiji, hivyo kufanya watoto wote kuhudhuria shule. Hata watoto wa makabila ya wahamaji huenda shule katika mazingira yao. Katika kusaidia hili, wazazi, Mfuko wa Jamii na mashirika ya kimataifa kama DANIDA, JICA, SIDA na baadhi ya mabenki yanachangia rasilimali zao kuunga mkonojuhudi za serikali.
Changamoto: Tufanye nini sasa kwene Mashule yetu
[hariri chanzo]Pamoja na programu nzuri tulizonazo, ukweli unabaki kuwa ni lazima Tanzania ifanye jambo ili kuwasaidia walemavu ambao hatimae nao wataweza kujisaidia na kuchangia katika pato la taifa lao. • Utumiaji wa madarasa hayo haukufikiriwa wakati wa kujenga shule na madarasa • Vifaa maalum na walimu havikuandaliwa tayari kwa watoto wasioona • Hakuna walimu wa kutosha wenye taaluma ya elimu maalum ya Viziwi, na wachache waliopo hawajui kutumia lugha ya ishara. • Changamoto hizo hizo wanakutana nazo watoto wenye ulemavu wa akili, viziwi vipofu
Elimu mjumuisho
[hariri chanzo].
Tanzania inajaribu kutekeleza mpango huu kulingana na tamko la Salamanca: 1994. Wizara ya Elimu inahamasisha wazazi kupeleka watoto wao walemavu shule maalumu.
Je, tuwachanganye Walemavu katika shule moja kama suluhisho?
Wengi wa Walemavu wanapendelea shule za elimu maalum, lakini hukiri pia kwamba hakuna shule za kutosha, na zilizopo zinaendeshwa na misaada.Basi makubaliano ni kwamba ni vizuri kuwa na shule za mjumuisho kuliko kukosa kabisa.
Shule mjumuisho zinakubalika, kwa kufuata haya: • Upatikanaji wa huduma kwa wenye ulemavu wa kimwili • Elimu maalumu kwa wasioona kutoka darasa 1-3, halafu darasa mjumuisho kutoka daraja 4 kwa vipofu • Kwa Viziwi na Viziwi vipofu, madarasa jumuishi si ya vitendo!
Watahitaji madarasa na walimu maalum kwa wanaofahamu lugha ya ishara. Mahitaji yao ya kimawasiliano huleta ugumu kwao kusoma kwenye darasa moja, hasa kwa shule za msingi.
• Watoto wanaoweza kufaidika katika darasa mjumuisho ni kwa wale wenye matatizo ya kusikia kidogo. Kwa wale ambao ni bubu kabisa ni kupoteza muda na rasilimali kuwaweka katika darasa mjumuisho. • Inakubalika kwamba kwa sekondari na elimu ya juu wakalimani wanaweza kutumika katika darasa mjumuisho. Katika hatua hii hawana ujuzi wa lugha-ishara kumwelewa mkalimani.