Wikipedia:AfroCrowd 2025/Ripoti
Ujenzi wa maarifa kwa washiriki
[hariri chanzo]Afrika Yetu, Utamaduni Wetu
[hariri chanzo]Mnamo tarehe 5 Julai, 2025 tulifungua tukio letu la kwanza la AfroCrowd kwa lengo la kuboresha makala za Wikipedia. Tukio hili lilifuata kalenda yetu ya matukio ya mwaka mzima kama tulivyoainisha katika maombi yetu ya General Support Fund. Tulikusanyika pale SeedSpace kuanzia saa tano asubuhi hadi saa jioni. Katika hafla hii tulipata washiriki wasiopungua 22. Ijapokuwa idadi tulitaka ishirini pekee. Kumi na tisa katika hao walikuwa na vifaa hivyo waliweza kujisajaili katika dashibodi (https://outreachdashboard.wmflabs.org/courses/Jenga_Wikipedia_ya_Kiswahili/AfroCrowd_Afrika_Yetu_Utamaduni_Wetu_(July_5,_2025).
- Aina za makala
Katika kufanikisha zoezi hili, tulizipanga makala katika maeneo mbalimbali. Maeneo hayo ni pamoja na;
- Historia
- Utamaduni
- Siasa
- Mapishi na,
- Makabila ya Afrika - (kama ziada baada ya kumaliza mpango kazi ndani ya muda).
Orodha halisi haikuchukua muda, kikosi kazi tulichokipa mafunzo kilimaliza kuboresha makala za historia ya Afrika nzima. Wakaendelea hadi upande wa utamaduni (mfano: https://sw.wikipedia.org/wiki/Utamaduni_wa_Angola), siasa (makala ya mfano: https://sw.wikipedia.org/wiki/Siasa_ya_Kamerun), mapishi (makaala ya mfano: https://sw.wikipedia.org/wiki/Mapishi_ya_Angola) na mwishowe tukadondokea katika makabila. Kupata orodha nzima ya kazi zilizofanywa, tazama hapa: https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:AfroCrowd_2025/Makala
Takwimu
[hariri chanzo]Wikipedia
[hariri chanzo]Kwa kile kilichofanyika katika Wikipedia ya Kiswahili ni kama ifuatavyo;
| Takwimu | Idadi |
|---|---|
| Makala zilizoundwa | 331 |
| Makala zilizohaririwa | 567 |
| Jumla ya uhariri | 1.58K |
| Baiti zilizoongezwa | 852K |
| Marejeo yaliyoongezwa | 1.1K |
Wikidata
[hariri chanzo]| Kundi | Hatua | Idadi |
|---|---|---|
| Jumla | Marekebisho yote | 108 |
| Jumla | Viungo vya kati ya wiki vilivyoongezwa | 74 |
| Vitu | Vilivyoundwa | 4 |
| Lebo | Zilizo ongezwa | 16 |
| Maelezo | Yaliyo ongezwa | 13 |
| Vifananisho (Aliases) | Vilioongezwa | 6 |
Picha za tukio
[hariri chanzo]Tukio la Pili, Afrika Yetu, Kamusi Yetu - Wikamusi
[hariri chanzo]Editathon ilifanyika mnamo tarehe 16 Agosti, 2025. Tukio hili linahitisha robo ya kwanza ya kalenda ya mwaka mzima ya matukio yaliyopangwa kutekelezwa na Jenga Wikipedia ya Kiswahili kwa mwaka wa 2025-2026. Katika tukio hili, tulihamia katika mradi ndugu wa Wikamusi ambao pia ni sehemu ya miradi ya Wikimediaa Foundation. Mradi huu si maarufu sana (kwa baadhi ya watu) kama jinsi ilivyo Wikipedia.
Kwa kuongeza pia, mradi huu kwa namna moja au nyingine - umetelekezwa kiasi fulani. Sasa katika ahadi zetu, tulipanga kuirudisha katika hali ya uhai wake. Kwanza kabisa kwa kuhakikisha tunaweka shughuli nyingi za kutoka kwa mwaka mzima. Ufunguzi huu wa tukio lake la kwanza tangu 2025, tumepata zaidi ya ingizo 14300 na kitu.
Siku ya tukio, mradi ulikuwa na ingizo zipatazo 15,926 leo hii mradi upo kwenye 30,000 na kitu. Takribani ingizo elfu kumi tano (15,000) ndani ya mwezi. Tazama dashibodi: https://outreachdashboard.wmflabs.org/courses/Jenga_Wikipedia_ya_Kiswahili/AfroCrowd_-_Afrika_Yetu,_Kamusi_Yetu
Mbinu
[hariri chanzo]Njia tuliyoitumia kufikisha kiwango hicho, ni kuweka kama shindano lisilo rasmi ili kufukuzia ingizo 1,000. Mambo yakawa tofauti. Tulipofika 1000, nikasimamisha kuweka kama shindano. Badala yake, nikawashawishi vijana wafanye kazi kwa roho ya harakazi za Wikimedia (kujitolea). Kati ya hao, ninaweza kuwataja wachache walionyesha kiwango kikubwa cha uchapaji kazi. Yafuatayo ni majina ya washiriki waliovunja rekodi ya kuundaji ingizo nyingi zaidi.
| Na. | Jina la mtumiaji | Idadi ya ingizo | Maelezo |
|---|---|---|---|
| 1 | User:Bycashtz | 10,891 | |
| 2 | User:Tumaini Mwenda Ruleju | 3,284 | |
| 3 | User:E.Mazwa | 463 |
Katika orodha hiyo, kuna wengi wamefanya kazi kubwa lakini Bycashtz amesema pale Wikamusi amefika. Cha zaidi alichoomba kwangu ni kumuwezesha bando la intaneti kwa kadiri litakapojitajika. Anajitolea kuhariri ingizo za kutosha. Hilo ni zoezi lake endelevu hadi hapo atakapoanza chuo!
Takwimu
[hariri chanzo]Kwa vile theme ya wakati huu isingetosha kufikisha malengo ya awali ya ingizo 1000, ilibidi tuwaache washiriki huru kuingiza yale wanayoona wanayaweza. Ifuatayo ni takwimu kamili.
| Takwimu | Idadi |
|---|---|
| Kurasa zilizoundwa | 14.3K |
| Kurasa zilizohaririwa | 14.7K |
| Jumla ya hariri | 15K |
| Wahariri | 28 |
| Baiti zilizoongezwa | 3.77M |
| Marejeo yaliyoongezwa | 0 |