Wete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Wete
Wete is located in Tanzania
Wete
Wete
Mahali pa mji wa Wete katika Tanzania
Anwani ya kijiografia: 5°3′36″S 39°42′36″E / 5.06°S 39.71°E / -5.06; 39.71
Nchi Tanzania
Mkoa Pemba Kaskazini
Wilaya Wete
Ramani ya Wete (Pemba)
Mahali pa Wete katika Pemba

Wete ni mji katika kaskazini ya kisiwa cha Pemba. Ikiwa ina wakazi 29,000 ni mji mkubwa wa Pemba pia makao makuu ya Mkoa wa Pemba Kaskazini na pia ya Wilaya ya Wete.

Umbali na Chake Chake ni kilomita 20.

Bunge la Zanzibar lina jengo hapa Wete linalotumiwa kwa ajili ya mikutano ya bunge kisiwani Pemba.

Bandari ya Wete ilikuwa muhimu lakini haifai kwa meli kubwa tena haikutengenezwa tena ipasavyo baada ya kujengwa kwa bandari ya Mkoani. Lakini bado karafuu kutoka kaskazini ya Pemba zasafirishwa kupitia bandari ya Wete.

Kuna hospitali. Maghofu ya jumba la Mtambwe Mkuu yako kwenye kisiwa kidogo karibu na Wete.

Mauaji ya Wete 2001[hariri | hariri chanzo]

Katika chaguzi za vyama vingi tangu mwaka 1995 wakazi wengi wa Wete jinsi wakazi wa Pemba kwa jumla walipendelea chama cha CUF. Kiongozi wa CUF Seif Shariff Hamad ni mwenyeji wa Wete. Baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 wafuasi wa CUF waliona ya kwamba kura haikuwa ya kweli na tar. 27 Januari 2001 maelfu ya wananchi walikusanyika Wete kudai uchaguzi urudiwe.

Askari za Polisi walikuwa na amri kuzuia maandamano yalivunjwa na polisi kwa ukali mkubwa. Waandamanaji angalau 13 waliuawa, watu 213 walijeruhiwa na zaidi ya 400 walikamatwa. Polisi pamoja iliendelea kutafuta wapinzani katika siku zilizofuata kuna taarifa ya kwamba watu wengi walipigwa na wanawake kunajisiwa. Zaidi ya watu 2,000 kutoka Pemba walikimbia Kenya kwa maboti madogo walipoishi katika makambi hasa shimoni.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Taarifa ya Human Rights Watch juu ya mauaji ya 2001 mjini Wete na Pemba kwa jumla