Wavisigoti


Wavisigoti (yaani Wagoti wa Magharibi) walikuwa kabila la Kigermanik, ambalo pamoja na Waostrogoti, walichangia sana anguko la Dola la Roma na mwanzo wa Karne za Kati Ulaya.
Historia[hariri | hariri chanzo]
Wakitokea labda Uswidi, wanatajwa na waandishi wa Roma ya Kale kama wakazi wa beseni la Vistula (leo Polandi Kaskazini) katika karne ya 1. Baadaye walienea kwenye Bahari Nyeusi, walipowazidi Wasarmatia kama watawala wa Mbuga za Ponto wakaanza kushambulia maeneo ya Dola la Roma hadi Cyprus.
Wakati huo waligawanyika kati ya Wathervingi na Wagreuthungi. Miaka ya 300, Ermanariki, mfalme wa Wagreuthungi, alitawala kutoka Bahari ya Baltiki hadi Bahari Nyeusi, na Milima ya Urali. Wakati huo wengi wao waliingia Ukristo wa madhehebu ya Uario kwa umisionari wa Ulfilas, aliyebuni alfabeti ya Kigoti kuandika Biblia ya Kigoti.
Miaka ya 370 maeneo ya Wagoti yalivamiwa na Wahunni. Wagreuthungi wakakaa chini yao wakaja kuitwa Waostrogoti, kumbe Wathervingi, waliojulikana baadaye kama Wavisigoti, walivuka mto Danube na kuvamia Dola la Roma. Baada ya kunyanyaswa sana, waliasi na kushinda Warumi katika Mapigano ya Adrianopoli mwaka 378. Chini ya Alariki I, waliteka Roma yenyewe mwaka 410, na hatimaye wakalowea Galia na Hispania, walipounda Ufalme wa Wavisigoti.
Wakiungana na Dola la Roma Magharibi dhidi ya Wahunni wa Attila na Waostrogoti walipata ushindi kwenye Mapigano ya Mabonde ya Katalunya mwaka 451. Hapo Waostrogoti walijinasua katika utawala wa Wahunni wakavamia Italia mwishoni mwa karne ya 5 chini ya mfalme Theodoriki Mkuu, wakaanzisha Ufalme wa Waostrogoti hadi mwaka 535 waliposhindwa na Kaisari Justinian I.
Ufalme wa Wavisigoti ulidumu hadi mwaka 711, ulipoangamizwa na Waislamu wa ukhalifa wa Umayyad. Kaskazini mwa Hispania, mabaki ya Wavisigoti chini ya Pelagius wa Asturias walianzisha Ufalme wa Asturias na kujiandaa kutwaa tena rasi yote (Reconquista).
Wazalendo wa Hispania walidai kuwa wazao wa Wagoti.
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Arce, Javier (1999). "The City of Merida (Emerita) in the Vitas Patrum Emeritensium (Vith Century)", East and West, Modes of Communication: Proceedings of the First Plenary Conference at Merida Vol. 5 [Transformation of the Roman World]. Leiden: Brill. ISBN 978-9-00410-929-2.
- Burns, Thomas (2003). Rome and the Barbarians, 100 B.C.–A.D. 400. Johns Hopkins University Press. ISBN 978-0-80187-306-5.
- Bury, J. B. (2000). The Invasion of Europe by the Barbarians. W.W. Norton & Company. ISBN 978-0-39300-388-8.
- Carr, Karen (2004). "Visigoths", Ancient Europe, 8000 B.C.–A.D. 1000: Encyclopedia of the Barbarian World Vol. 2 [Bronze Age to Early Middle Ages]. New York: Thomson Gale. ISBN 0-684-31421-5.
- Claude, Dietrich (1998). "Remarks to the Relationship between Visigoths and Hispano-Romans in the 7th Century", Strategies of Distinction: Construction of Ethnic Communities, 300–800 (The Transformation of the Roman World, vol. 2). Leiden: Brill Academic Publishers. ISBN 978-9-00410-846-2.
- Collins, Roger (1992). Law, Culture, and Regionalism in Early Medieval Spain. Variorum. ISBN 0-86078-308-1.
- Collins, Roger (1995). The Arab Conquest of Spain, 710–797. Blackwell Publishers. ISBN 978-0-63119-405-7.
- Collins, Roger (1999). Early Medieval Europe, 300–1000. Palgrave Macmillan. ISBN 978-0-33365-808-6.
- Collins, Roger (2000). "Visigothic Spain, 409–711", in Raymond Carr: Spain: A History. New York: Oxford University Press. ISBN 978-0-19280-236-1.
- Collins, Roger (2004). Visigothic Spain, 409–711. Blackwell Publishing. ISBN 0-631-18185-7.
- Coolidge, Grace (2011). Guardianship, Gender, and the Nobility in Early Modern Spain. Ashgate. ISBN 978-1-40940-053-0.
- Durant, Will (1950). The Age of Faith, The Story of Civilization IV. New York: Simon and Schuster.
- Fletcher, Richard (2006). Moorish Spain. University of California Press. ISBN 978-0-52024-840-3.
- Frassetto, Michael (2003). Encyclopedia of Barbarian Europe: Society in Transformation. ABC-CLIO. ISBN 978-1-57607-263-9.
- Fuller, J.F.C. (1998). Armaments & History. Da Capo Press. ISBN 978-0-30680-859-3.
- Georgescu, Vlad (1991). The Romanians. A History. Ohio State University Press. ISBN 0814205119.
- Gerber, Jane (1992). The Jews of Spain: A History of the Sephardic Experience. Free Press. ISBN 978-0-02911-573-2.
- Gonzalez-Salinero, Raul (1999). "Catholic Anti-Judaism in Visigothic Spain", in Alberto Ferreiro: The Visigoths: Studies in Culture and Society. Leiden: Brill. ISBN 978-9-00411-206-3.
- Graetz, Heinrich (1894). History of the Jews Vol. III [From the Revolt Against the Zendik (511 CE) to the Capture of St. Jean D'acre By the Mahometans (1291 C. E.)]. The Jewish Publication Society of America.
- Halsall, Guy (2007). Barbarian Migrations and the Roman West, 376–568. Cambridge University Press. ISBN 978-0-52143-543-7.
- Heather, Peter (1998). The Goths. Blackwell Publishers.
- Heather, Peter (2005). The Fall of the Roman Empire: A New History of Rome and the Barbarians. Oxford University Press. ISBN 978-0-19515-954-7.
- Heather, Peter (2013). The Restoration of Rome: Barbarian Popes and Imperial Pretenders. Oxford University Press. ISBN 978-0-19936-851-8.
- Hillgarth, J. N. (2010). The Visigoths in History and Legend. Brepols Publishers. ISBN 978-0-88844-166-9.
- James, Edward (2009). Europe's Barbarians AD 200–600. Routledge. ISBN 978-0-58277-296-0.
- Katz, Solomon (1955). The Decline of Rome and the Rise of Mediaeval Europe. Cornell University Press.
- Lim, Richard (1999). "Christian Triumph and Controversy", Late Antiquity: A Guide to the Postclassical World. Cambridge, MA: The Belknap Press of Harvard University Press. ISBN 978-0-67451-173-6.
- (1999) "Forging a New Identity: The Kingdom of Toulouse and the Frontiers of Aquitania, 418–507", in Alberto Ferreiro: The Visigoths: Studies in Culture and Society. Brill. ISBN 978-9-00411-206-3.
- (2013) The Story of Spanish. New York: St. Martin's Press. ISBN 978-0-31265-602-7.
- Odobescu, Alexandru (1889). Le Trésor de Pétrossa. Étude sur l'orfèvrerie antique. Éditions J. Rothschchild.
- Ostler, Nicholas (2006). Empires of the Word: A Language History of the World. Harper Perennial. ISBN 978-0-06093-572-6.
- Roberts, J. M. (1997). A History of Europe. Allen Lane. ISBN 978-0-96584-319-5.
- Roth, Norman (1994). Jews, Visigoths, and Muslims in Medieval Spain: Cooperation and Conflict. Brill. ISBN 978-9-00409-971-5.
- Sarris, Peter (2002). "The Eastern Roman Empire from Constantine to Heraclius, 306–641", in Cyril Mango: The Oxford History of Byzantium. New York: Oxford University Press. ISBN 978-0-19814-098-6.
- Sivan, Hagith (1987). "On Foederati, Hospitalitas, and the Settlement of the Goths in A.D. 418". American Journal of Philology 108 (4): 759–772.
. https://archive.org/details/sim_american-journal-of-philology_winter-1987_108_4/page/759.
- Stevenson, W. H. (1899). "The Beginnings of Wessex". The English Historical Review (Oxford, UK: Oxford University Press) 14 (53): 32–46. https://zenodo.org/record/2217573/files/article.pdf.
- Todd, Malcolm (2000). The Early Germans. Blackwell. ISBN 978-0-63119-904-5.
- (2006) Encyclopedia of European Peoples. New York: Facts on File. ISBN 978-0816049646.
- Williams, Mark (2004). The Story of Spain. San Mateo, CA: Golden Era Books. ISBN 978-0-97069-692-2.
- Wolf, Kenneth Baxter (2014). Christian Martyrs in Muslim Spain. Cambridge and New York: Cambridge University Press. ISBN 978-1-10763-481-7.
- Wolfram, Herwig (1988). History of the Goths. University of California Press. ISBN 978-0-52005-259-8.
- Wolfram, Herwig (1997). The Roman Empire and its Germanic Peoples. University of California Press. ISBN 0-520-08511-6.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wavisigoti kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |