Wassily Kandinsky
Wassily Kandinsky [1] (16 Desemba 1866 - 13 Desemba 1944) alikuwa mchoraji kutoka nchini Urusi na mtaalamu wa nadharia ya sanaa.
Anahesabiwa kati ya wasanii muhimu zaidi wa karne ya 20. Alikuwa mkubwa katika sanaa ya kisasa kwenye mwanzo wa karne ya 20 akaumba taswira ambazo ni kati ya kazi za kwanza za sanaa isiyoshikika (abstract art) [2]. Sanaa yake ilibadilika mara kadhaa wakati wa maisha yake.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Moscow lakini miaka ya utoto wake aliishi huko Odessa kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Moscow akasoma sheria na uchumi. Alifanikiwa kabisa katika taaluma yake - alialikwa kuwa profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dorpat - alianza kuchora akiwa na umri wa miaka 30.
Mnamo 1896 alihamia Munich (Bavaria - Ujerumani) na kusoma kwanza katika shule ya binafsi, kisha katika Chuo cha Sanaa cha Munich. Alirudi Moscow mnamo 1914 baada ya mwanzo wa Vita ya Kwanza ya Dunia. Hakupendezwa na mafundisho rasmi ya kufundisha sanaa baada ya mapinduzi ya Urusi akarudi Ujerumani mnamo 1921. Huko alifundisha katika shule ya sanaa na usanifu Bauhaus kuanzia 1922 hadi 1833 wakati Wanazi walipokifunga. Kisha alihamia Ufaransa ambako aliishi maisha yake yote, na kupata kuwa raia wa Ufaransa mnamo 1939. Alifariki huko Neuilly-sur-Seine mnamo 1944.
Vipindi vya kisanii
[hariri | hariri chanzo]- 1 Kijana na msukumo (1866-1896)
- 2 Metamofosisi
- 3 Kipindi cha Mpanda Farasi Buluu (1911-1914)
- 4 Kurudi Urusi (1914-1921)
- 5 Bauhaus (1922-1933)
- 6 Usanisi Mkubwa (1934-1944)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Amazon inayoendesha, 1911
-
Fugue, 1914
-
Schilderij Blick a Murnau mit Kirche, 1920
-
Kandinsky ya The Ark kuonyeshwa nje ya makumbusho katika Genoa
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tamka 'Vassily', lakini alichagua mwenyewe tahajia ya Kijerumani (kwa Kirusi: Василий Кандинский)
- ↑ Manierre Dawson may have been the first: Ploog, Randy J., Myra Bairstow and Ani Boyajian 2011. Manierre Dawson (1887-1969): a catalogue raisonné. The Three Graces in association with Hollis Taggart Galleries, New York.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wassily Kandinsky kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |