Wasangu (Tanzania)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wasangu ni kabila kutoka eneo la nyanda za juu kusini-magharibi la nchi ya Tanzania. Mwaka 1987 idadi ya Wasangu ilikadiriwa kuwa 75,000, Lugha yao ni Kisangu.

Jamii ya Wasangu[hariri | hariri chanzo]

Makala haya yanazungumzia habari za Wasangu waishio katika bonde la Usangu katika Wilaya Mbarali, mkoa wa Mbeya. Habari nyingi juu yao zimesahauliwa kwa sababu hakuna mtu aliyejishughulisha kuzitafuta na kuzihifadhi.

Bonde la Usangu[hariri | hariri chanzo]

Jumla ya Wakaaji wa bonde la Usangu ni zaidi ya watu 74,000 Kama ilivyohesabiwa mwaka 1972. Lakini jumla ya watu kamaSerikali ilivyohesabu mwaka 1967 ni watu 56,743, kwahiyo jumla ya watu katika bonde la Wasangu yaongezeka kwa haraka sana kuliko jumla ya watu inavyoongezeka katika sehemu zingine za Tanzania. Sababu zinazofanya watu waongezeke upesi sana katika bonde hili ni nyingi sana; na baadhi yasababu zenyewe ni kama hizi hapa chini:

Sababu ya kwanza ni kwamba bonde hili la Usangu tangu zamani lilikuwa halijulikani sawasawa na watu wengi jinsi lilivyo na manufaa kwa shughuli mbali mbali za uzalishaji mali kwa sababu Wasangu walikuwa wapiganaji hodari wa vita kwa hiyo ilikuwa ni vigumu sana kwa jatnii zingine kwenda kufanya mastaakimu yao huko. Hata baada ya Wakoloni kukomesha vita vya jamii mbalimbali za Nyanda za juu za Kusini, jamii zilikuwa hazijui habari kamili kuhusu bonde hili. Baada ya Uhuru tu, mawasiliano katika bonde hili na nje ya mbugaza Usangu yakabadilika sana na kuwa bora zaidi yaliyoletwa na Chama cha TANU katika kuhudumia watu wake sawasawa. Pili, udongo wa mbuga za Usangu ni nzuri sana kwa hiyo mkulima halazimiki kutia mbolea hata kidogo katika mashamba yake. Mbolea ya asili ni nyingi mno katika udongo na mimea ikipandwa hustawi sana. Tatu, kuna mito mingi yenye maji kwa matumizi ya watu na mifugo pia, kwa hiyo watu wamevutiwa sana na mali ya asili ya namna hii. Nne, Mbuga za Usangu zinafaa sana kwa ufugaji wa mifugo — hasa ng'ombe, mbuzi na kondoo. Majani yanapatikana kwa urahisi na maji kwa ajili ya mifugo kwa hiyo wafugaji wamevutiwa sana na mbuga hizi kutoka wilaya za jirani na za mbali pia. Tano, mbuga za Usangu ni kubwa sana na zina nafasi kubwa za kustawisha malisho ya mifugo na ulimaji wa mazao mbalimbali. Mvua zanyesha kiasi cha kutosha bali kuna jua kali sana wakati wa kiangazi. Hali kadhalika ziko sababu zingine nyingi zilizowavutia watu kuja kukaa katika mbuga za Usangu toka Mikoa mingine.

Jamii zinazoishi katika bonde la Usangu ni Wasangu ambao ni wenyeji wa mbugaza Usangu Wanyakyusa ambao wamehamia mbuga za Usangu toka Rungwe kuja kulima mashamba ya mpunga na mimea mingine; Wabena ambao wamehamia mbuga hizo toka Wilaya ya Njombe na hushughulika zaidi na kilimo cha mpunga na mazao mengineyo. Wakinga toka Wilaya ya Njombe, nao hujishughulisha sana na biashara — hasa biashara ya samaki; Wahehe toka Wilaya ya Iringa — hujishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji; Wahehe wanafanana sana na Wasangu katika mila na desturi; Wamasai na Wasukuma, ambao hasa walianza kuhamia katika mbuga za Usangu tangu mwaka1973, mwezi Septemba. Jamii hizi mbili zimehamia mbugaza Usangu juzi juzi tu, lakini jamii zingine zilihamia mbuga za Usangu miaka mingi kidogo iliyokwisha pita. Wamasai hujishughulisha zaidi na ufugaji na Wasukuma hujishughulisha na mambo yote mawili, ufugaji na ukulima. Jamii nyingine ambayo imekaa sana katika bonde la Usangu ni jamii ya Wabaluchi ambao wanaitwa kama "Maburushi".

Jamii hii imekaa katika mbuga za Usangu tangu karne ya 19 na tangu wakati huo jamii hii imejishughulisha sana na kilimo cha mpunga na pia mazao mengine. Walikuwa watu wa kwanza katika bonde ia Usangu Kutumia kilimo cha kumwagilia maji katika mashamba kwa njia ya mifereji iliyochimbwatoka mto Mbarali. Angalia habari zao hapa chini.

Udongo wa Ubonde wa Usangu[hariri | hariri chanzo]

Bonde la Usangu lilikuwa na mi to ambayo maji yake yalikuwa yanatiririkia kuelekea katika bonde la Ziwa Rukwa naZiwa Nyasa. Milipuko ya Volkano ya mlima Rungwe ikaizuia mito hiyo kwa mwinuko wa ardhi halafu mito ikatiririka katika bonde la Usangu na kulifanya bonde la Usangu kuwa ziwa. Katika mabadiliko ya ardhi, udongo, changarawe na michanga ikaletwachini yaziwa lenyewe.

Mito ambayo ilikuwa inatiririkia katika bonde la ziwa Rukwa na ziwa Nyasa, sasaziwa lililokuwapo katika bonde la Usangu (mahali ambapo mbuga za Usangu zipo sasa) likapata nafasi ya kuyamwaga maji yote kwa njia ya mito upande wa Kaskazini-Mashariki, na mbuga zikatokea toka kwenye mchanga wa ziwa lenyewe. Na udongo na matope na udongo wa mfinyanzi unaopatikana katika mbuga za Usangu umeletwa na mito mbali mbali inayotiririkia katike. bonde hili la Usangu. Udongo wa mbuga za Usangu ni wa aina nyingi na unafaa sana kwa mazao. Kuna udongo wa mfinyanzi, udongo wa mbuga, na udongo mweusi wenye rutuba sana. Udongo waainazote hizi una rutuba nyingi sana kwa mazao.

Mazao yapandwayo katika bonde hili ni mpunga, mahindi, viazi vitamu, viazi ulaya, ulezi, migomba, maharage, karanga, miwa, mihogo na maboga mbalimbali.

Magonjwa[hariri | hariri chanzo]

Mbuga za Usangu zina maradhi mengi sana, magonjwa ambayo yanawasumbua sana watu ni homa, kichocho, safura, surua, homa ya papasi, ugonjwa wa kuhara na magonjwa ya minyoo ya aina mbalimbali. Walakini magonjwa mabaya sana ambayo yanammalizia mkulima wakati wake mwingi sana ni kichocho, homa, safura na ugonjwa wa kuhara. Sababu ya kupatikana kichocho kwa wingi sana katika mbuga za Usangu ni kwamba mbuga za Usangu zina matopematope mengi sana na pia kuna majimaji mengi ambayo yamekwama hayatembei.

Konokono ambao ndio hueneza vidudu vya ugonjwa wa kichocho hupenda sana kuogelea katika maji ambayo yamekwama na kwa jinsi hii vidudu vya kichocho huachwa humohumo majini vikingojea mwanadamu yeyote kupitia katika maji hayo au kuogelea katika maji hayo na wakati huo vidudu ya kichocho vyamrukia mtu na kupenyeza katika mwili wake hadi kibofuni na kwenye matumbo ambako vyazaliana sana na kuanza kula sehemu ya gozi ya sehemu hizo.

Kuutibu ugonjwa wa kichocho ni kazi ngumu sana lakini waweza kuzuiliwa kwa urahisi sana kwa kutumia njia zilizo rahisi sana za kiafya.

Ugonjwa mwingine unaowasumbua sana watu waishio katika mbuga hizi ni homa ya mbu. Mbu nao huzaliana kwa wingi sana kwa sababu ya unyevunyevu mwingi unaopatikana katika mbuga hizi — hasa katika mashamba ya mpunga ambayo yana maji ya kumwagilia mashamba yakaayo kwa muda mrefu hata kuwawezesha mbu kuzaliana kwa muda mrefu sana. Penye maji yaliyosimama ndipo mbu huzaliana haraka sana na kwa urahisi mno. Kama nilivyosema hapo juu, mbuga za Usangu zina matopematope mengi na madimbwimadimbwi mengi yaliyokwama ambayo yanafaa sana kwa mbu kuzaliana.

Ugonjwa mwingine wa watu wa Usangu unaowasumbua sana ni ugonjwa wa kuhara. Ugonjwa huu watokana na kunywa maji machafu, na mbuga za Usangu nyingi zina maji yaliyo machafu na hayafai kunywa binadamu.

Lakini watu hawana njia nyingine ya kupatia maji yaliyo safi isipokuwa hiyo tu. Maji ya mto ambayo ni maji safi kidogo kuliko maji aliyotuama yanapitia kwa mbali sana na ni watu wachache tu wanaonufaika na maji haya ambazo wanaishi karibu ya hiyo mito.

Kwa sasa hivi Wizara ya Afya inatoa mafunzo ya afya kwa akina mama walio karibu na kituo cha afya cha Rujewa na vijiji vingine. Pia kituo hicho kinatoa dawa za kukinga maradhi ya surua, kifaduro, ndui, polio na kifua kikuu. Tatizo kubwa kwa upande wa utumishi ni kwamba wafanyakazi ni wachache sana.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wasangu ni watu ambao wanahusiana na jamii za Kihehe, Kisafwa, Kibena, Kinyakyusa na kidogo jamii ya Kingoni. Jamii zote hizi, isipokuwa Wangoni, ni jirani za Wasangu, na kwa jumla Wasangu walikuwa watu ambao walijulikana sana katika nyanda za juu za Kusini katika karne ya 18 na karne ya 19. Hali kadhalika walikuwa ni jamii iliyokuwa na nguvu nyingi sana ya utawala na kivita. Hawa watu walikuwa wanaishi sehemu ya llamba iliyo karibu maili 60 Kaskazini ya Utengule kabla ya kuja Waarabu na Wajerumani, na kila mahali walipofanya maskani yao walipaita "Utengule", mahali pa amani.

Waarabu walipokuwa wanaingia katika nchi ya Usangu waliingia kufanya biashara. Hawa Waarabu walikuwa wanauza nguo, magobole, baruti na shanga. Kutoka kwa Wasangu, Waarabu walipata meno ya tembo. Hapo awali mbuga zote za Usangu zilikuwa na wanyama wa kila aina na ndovu walienea kila mahali katika mbuga hizi za Usangu, kwa hiyo ilikuwa rahisi sana kwa Wasangu kuwaua tembo na kupata meno yao ili wayauze kwa Waarabu.

Biashara nyingine kubwa ambayo ilikuwa inafanywa na Waarabu katika mbuga hizi za Usangu ilikuwa biashara ya utumwa. Wasangu walikuwa ni watu ambao walijua namna ya kupigana vita sawasawa na kwa kuwa walikuwa na chifu wao mmoja tu ilikuwa rahisi kwao kuungana pamoja na kufanya jeshi moja kali na lenye nguvu sana kuliko jamii zingine walizopakana nazo ambazo zilikuwa hazina utawala mmoja kama vile Wanyakyusa, Wasafwa na kadhalika. Lakini Wahehe na Wakimbu walikuwa na utawala mmoja sawa kama Wasangu walivyokuwa.

Kwa kuwa utawala wa Wasangu ulikuwa na nguvu na umoja mkubwa, waliweza kupigana vita kwa nguvu moja na jamii zingine zilizokuwa jirani nao. Chifu Merere, ambaye ndiye aliyekuwa mtawala wa Wasangu, alikuwa mtawala shupavu na mpenda raia wake. Kwa kuwa alikuwa anapata silaha bora toka kwa Waarabu alipowauzia meno ya tembo, aliweza kuwashinda maadui zake bila taabu kubwa na mateka waliuzwa kwa Waarabu wafanya biashara ya utumwa.

Hasa Merere aliwauza utumwani watoto wa Kisafwa na Kihehe ambao aliwateka wakati wa vita. Uwezo wake Merere katika kupigana na jirani zake ulisaidiwa sana na ushauri aliokuwa anaupata toka kwa wazee wa Kisangu na pia toka Mbaluchi ambaye alikwenda Usangu na kuwa Mshauri Mkuu wa Vita wa Chifu Merere I ambaye yaaminiwaaliingia nchi ya Usangu kati yamwaka1878 na mwaka1880. Mbaluchi (Mburushi) huyu aliitwa Jemadari ambaye kufika kwake Utengule/Usangu kulisababisha Wabaluchi wengine kuja Usangu na kuanza shughuli za kilimo cha mpunga (angalia chini ya kilimo hapa chini). Wasangu wenyewe wanasimulia kuwa Waarabu walianza kuingia nchi ya Usangu wakati wa utawala wa Chifu Njali aliyewazaa akina Merere.

siri na kupita huko. Si njia ya kutoka pwani tu iliyohatarishwa na Wasangu ball hata njia ya kuelekea nchi ya Wabemba kuelekea Zambia ilitiwa msukosuko.

Mara kwa mara Wasangu waliuteka utawala wa Kiwele uliokuwa sehemu ya kati ya Ukimbu ambao ulikuwa njiani Kusini ya Tabora. Mara baada ya Chifu Kilanga kutawala katika nchi ya Ubungu, Wasangu walimshambulia katika mwaka wa 1856 — 1857 wakimsaidia ndugu yake Kafwimbi, na ingawa Wasangu walishindwa, Kafwimbi alitorokea nchi ya Usangu tena. Kati ya mwaka 1859 wakati Bwana Burton alipoondoka Afrika ya Mashariki na mwaka 1866 Tippu Tip alipotembelea reli ya Usangu chifu Muigumba akafariki wakati akipigana na Wahehe.

Binini, ndugu ya Mihwela alikuwa amejifunza sana maarifa ya kupigana vita, na kwa kuwa alikuwa na ari kubwa ya kutaka kutawala Uhehe nzima. Wakati fulani karibu ya miaka ya 1860 alifanya vita na Wasangu na alifanikiwa kuviteka vijiji vingi sana na kuwateka wanawake na mifugo yao. Binini mwenyewe alimwua kiongozi wao Muigumba na akachukua jina lake na kujiita yeye mwenyewe Munyigumba kama ukumbusho wa ushindi wa kuwatawala Wahehe wote. Huyu Binini (Munyigumba) ndiye aliyekuwa baba wa chifu Mkwawa na ndiye chifu mkuu wa kwanza wa Wahehe wote.

Baada ya kifo cha Muigumba vita vikali sana vya urithi wa utawala vikatokea na mjukuu wake Muigumba kwa jina Merere Towelamahamba akatokea kuwa mshindi na akawaua jamaa zake wengi sana ambao alishindana nao katika kurithi utawala. Ugomvi wa urithi wa utawala uliwadhoofisha sana Wasangu katika kupigana vita na majirani zao.

Kati ya mwaka wa 1866 na mwaka wa 1872 Wasangu wakatokea jamii yenye nguvu sana chini ya chifu Merere wa kwanza kuliko hapo awali, na wakawashambulia majirani zao na kuziteka nchi zao zote hasa upande wa Mashariki Kusini na upande wa katikati wa nchi ya Wakimbu. Wakati huu Wasangu walikuwa wamefikia kilele cha nguvu zao na hakuna jamii nyingine yoyote iliyoweza kuikabili jamii ya Kisangu katika pande hizo za Tanzania.

Katika mwaka wa 1867 Bwana Livingstone aliambiwa na Waarabu katika nchi ya Ubungu kwamba Wasangu walikuwa ni wapole kwa wageni wowote, na kwamba Merere mara nyingi alifanya mashambulizi kwa machifu wa jirani ili ateke mifugo na watumwa na kuwauza kwa wafanya biashara wa Kiarabu. Katika mwezi wa Agosti Bwana Livingstone alisikia habari nyingi zaidi za kupendeza kuhusu chifu Merere na alichelea kuwa huenda akaharibiwa na Waarabu.

Walakini katika mwaka wa 1871 habari zikafika Mayema kwamba Merere kisha kosana na Waarabu akiwatuhumu kwamba walikuwa wanafanya njama ya kumshambulia ili Goambari, mmojawapo wa Wajukuu wa Muigumba aweze kutawala. Kwa ajili ya sababu hii Merere akawashambulia Waarabu na marafiki zao wote.

Akamwua Mwarabu mmoja akawanyang'anya Waarabu wengine mali yote waliyokuwa nayo.

Wakati huu Amrani Masudi akajitokeza kwenye uwanja wa vita. Amrani alikuwa Mwaarabu toka Zanzibar wakati Zanzibar ilipotawaliwa na Waarabu.

Tanzania Bara ilikuwa inatawaliwa na machifu mbalimbali wa jamii mbali mbali na Waarabu waliokuwa wakiishi Tanzania Bara walikuwa wafanya biashara tu sio watawala. Kwa jinsi hii Amrani hakupendelea utaratibu huu, kwa hiyo akaamua kuwafanyia vita machifu wote wa Tanzania Bara na kuwafanya watu wote wawe chini yake ili baadaye waweze kumletea meno ya tembo bila ya kuyalipia chochote.

Wakati Amrani Masudi alipofika Tabora akaambiwa kuwa kuna machifu wawili wenye nguvu sana ambao walihatarisha misafara yote ya biashara ya Waarabu na kuwatoza kodi kubwa kabla ya kuwaruhusu kupita katika nchi zao. Machifu wenyewe ni Nyungu-ya-Mawe wa Kiwele katika nchi ya Ukimbu na Merere wa Usangu. Lakini chifu wa hatari kabisa na mwenye nguvu zaidi kuliko mwenzake alikuwa Merere.

Baada ya kupata habari hizo, Amrani akalichukuwa jeshi lake na akaomba kuongezewa askari toka kwa machifu waliomwogopa kupigana naye ili aende na jeshi kubwa la kuweza kumshambulia Merere vilivyo. Alipoondoka Tabora, alipita Ngulu, Unyangwila, Itumba, Kipembawe na Igunda mpaka akafika Usangu. Maluteni wake walipita Ukonongo, Isamba, Wikangulu, Ubungu na Uguruke. Wengine walipitia Ugogo. Kila chifu wa sehemu za Magharibi na kati na Kusini ya Tanzania alitoa kwa Amrani askari wa kumsaidia katika vita kati yake na Wasangu. Lakini Nyungu-ya-Mawe hakutoa hata askari mmoja wa kumpa Bwana Amrani.

Wasafwa kutoka sehemu za Ukinga ni kwamba nchi ya Ukinga imeinuka sana na mwinuko huu huwagawanya watu kuwa katika pande mbili zilizo tofauti ya hali ya Kijiografia, hata baadaye watu ambao pengine asili yao ni moja kuwa katika jamii mbili zilizo tofauti kabisa, ambazo lugha zao zatofautiana.

Mambo yanapotokea hivi, basi kutoelewana kwaweza kutokea na kuchukiana pia kukatokea. Ngazi hii ikifikiwa basi kundi lisilotaka ugomvi huhamia mahali pengine ambapo kuna usalama zaidi na hali hii yawezekana kabisa iliwapata Wasafwa na kuamua kuhamia sehemu za Mbeya ambako maskani yao ya kudumu yalifanyika. Jamii ya Wasafwa yagawanyika katika jamii hizi kubwa:

(i) Wasongwe ambao huishi sehemu za mto Songwe;

(ii) Wamalila ambao wanaishi katika milima ya Umalila.

(iii) Wamporoto ambao huishi kwenye milima ya Mporoto.

(iv) Wambwila ambao huishi kati ya Wasongwe na Wasangu.

(v) Waguluhaambao huishi sehemu za lleya.

Kilimo[hariri | hariri chanzo]

Wasafwa walitumia majembe yao ya kwanza ambayo yalikuwa ya miti, yaani miti ilichongwa vizuri kabisa mithili ya jembe halafu wakayatumia kwa kulimia. Katika kuchonga majembe ya miti, tezo na mashoka yalitumiwa, zana ambazo zilikuwa za chuma kilichotengenezwa toka Ukinga. Pia zana hizi hizi, mashoka na tezo, zilitumika katika kuchongea mizinga ya nyuki.

Miti iitwayo 'Magambo' na miyombo ilifaa sana kutengenezea majembe. Mizinga ya nyuki ilichongwa kutokana na mti wowote ule.

Baadaye sana, majembe ya miti yakaonekana hayafai ndipo majembe ya chuma kutoka Ukinga yakatumiwa zaidi na kuonekana bora zaidi. Katika shughuli za kulima, kwanza walianza kulima mashamba ya chifu wao, yaani "Kwila", maana yake "Shamba la Chifu".

Baada ya hapo kila raia alikwenda kulima shamba lake. Walakini kualikana katika shughuli za kilimo lilikuwa jambo la kawaida ili mashamba yamalizike upesi.

Mtu alipotaka kualika wenziwe wamsaidie kulima mashamba yake, alipika pombe na chakula cha kutosha ili baada ya kulima watu waweze kula na kunywa pombe. Wale walioalikwa siku hiyo waliimba nyimbo wakati wa kula chakula na pia ngoma zilichezwa ili kuonyesha furaha kubwa ya chakula walichopewa.

Iwapo jamaa mmoja alitokea kutokuwa na chochote, yaani hana pombe wala chakula cha kuwapa watu watakaolima shamba lake, aliweza pia kuwaalika wenziwe hapo kijijini ili wamsaidie kulima na kumaliza shamba lake. Wanakijiji waliweza kulima shamba la mwenzao bure. Baada ya mavuno kupatikana basi huyo jamaa aliyelimiwa shamba lake bure aliweza sasa kupika pombe na chakula na kuwakaribisha wale wale jamaa waliomlimia shamba lake hapo awali ili kuonyesha shukrani zake kwa msaada aliopewa alipokuwa yeye hana kitu cha kuwapa. Ilikuwa desturi kwa kila mwanakijiji kukubali kualikwa na mwanakijiji yeyote, na kukataa kumsaidia mwanakijiji katika kulima ilikuwa ni mwiko. kitendo hiki cha kulimiwa shamba bure mtu anapokuwa hana pombe wala chakula kiliitwa "Alimishumiwa", maana yake wanalima bure bila kuwapa chochote cha kula wanaolima shamba la mtu siku hiyo. Siku hizi Wasafwa wanaalikana katika shughuli za kilimo lakini si sana kama ilivyokuwa hapo zamani.

Katika nchi ya Usafwa shughuli za kilimo zaendelea wakati wowote katika mwaka kwa sababu hali ya hewa na ya ardhi yaruhusu sana shughuli ya kilimo iweze kuendelea mwaka mzima, ingawa sehemu zingine za usafwa hazina bahati ya kuwa na hali hii ya hewa na rnanufaa mengine mengine ya kuendeleza hali ya kilimo. Kuna mazao ya aina nyingi sana ambayo hulimwa nyakati mbalimbali tofauti na mazao hayo hupandwa kwa kutegemea ardhi na jiografia ya mahali penyewe kwa sababu jiografia ya nchi ya Usafwa yahitilafiana toka mahali hadi pengine. Kilimo chao maalum ni cha sesa, lakini pia wanalima matuta, ufundi ambao wameigatoka kwa Wanyakyusa.

Watu wa Mporoto hulima matuta ya terrace ili kuzuia mmomonyoko wa udongo kando kando ya milima. Karibu robo moja ya wakulima wa Kisafwa hutumia trekta au plau laki ni matumizi ya zana hizi mbili hutegemea jiografia ya mahali shamba lilipo.

Mgawanyo wa kazi[hariri | hariri chanzo]

Katika jamii ya Kisafwa, baba huwa na shamba lake na mama huwa na shamba lake pia. Iwapo baba ametangulia kumaliza shamba lake huenda kumsaidia mkewe. Kufanya hivi hakumfanyi bwana adai sehemu yoyote juu ya umilikaji wa shamba na mali iliyomo katika shamba hilo. Bali husaidia tu kwa imani, lakini shamba labakia kuwa ni la mwanamke.

Kila mtu alikuwa na mamlaka juu ya shamba lake hata mavuno yake pia.

Mavuno kutoka shamba la baba ndilo lilifanya ghala ya chakula cha familia nzima.

Kama mke mmoja hakuvuna kiasi cha kutosha, basi mwanamke huyo aliweza kupata chakula toka ghala ya bwana yake. Lakini iwapo kila mwanamke ana chakula cha kutosha toka shambani mwake, basi bwana aliweza kuuza baadhi ya chakula toka kwenye ghala yake, ili kupata fedha za kununulia ng'ombe au mbuzi.

Pia mwanamke alikuwa haingiliwi na bwana wake katika umilikaji wa chakula. Alikuwa na uhuru kabisa wa kuweza kuuza chakula chake kama alipenda. Watoto walikitumia chakula toka kwa mama zao katika 'Ibanza' yao bila wasi wasi bila kujali mama ya nani kapika chakula hicho.

Lakini siku hizi ni vigumu kwa akina mama kulisha watoto wote sawa.

Hujali sana watoto wao tu; wamekuwa wachoyo na hawawezi kuwalisha watoto wa mwingine kama ambavyo wangaliwalisha watoto wao wenyewe. Ubinafsi umewaingia sana kitu ambacho hakikujulikana hapo zamani. Kabla ya kwenda kulima au kuvuna, mama hupika chakula asubuhi Hi waje wale mchana baada ya kazi. Umwagiliaji wa mashamba ulitumika kama Wasafwa wanavyotumia utaalamu huo kwa sasa. Mama, baba na watoto hulima pamoja.

Kuvuna[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa kuvuna, ngano hukatwa shina zima na kisu halafu hulundikwa pamoja. Baada ya kumaliza kuvuna, ngano yote hupigwa pigwa na mti (threshing) ili itoke kwenye masuke yake. Ulezi hukatwa vichwa vyake na kisu halafu huwekwa pamoja na baadaye huzitengeneza kwa kutenganisha punje zake toka kwenye masuke. Mahindi huvunwa kwa kukwanyua vigunzi vyake toka kwenye shina lake na kuwekwa pamoja. Kazi yote hii hufanywa kwa kualikana. Mtu mmoja peke yake alikuwa hawezi. Nyimbo ziliimbwa wakati wa kazi ya kuvuna na vyombo hivi, "Indili, Izeze, na Marimba" yalitumika katika kuwatumbuiza wafanyakazi.

Ghala[hariri | hariri chanzo]

Chakula kilihifadhiwa katika ghala maalum zilizotengenezwa kwa kazi hiyo. Ulezi na ngano vilihifadhiwa katika vilindo vikubwa vilivyoteng enezwa kwa kusuka matete pamoja kwa kutumia kamba za miyombo ambayo zama hizo zilipatikana kwa wingi karibu karibu na vijiji vyao. Mpaka sasa njia hii ya kuhifadhi mazao yatumika Usafwani kote.

Mahindi yalivunwa na kuanikwa penye uchanja kwanza ili yapate kukauka sawasawa. Baada ya hapo, mahindi yaliwekwa ndani ya kihenge kilichojengwa nje ya nyumba ya kulala. Hii ndiyo iliyokuwa ghala ya mahindi. Zamani hakukuwa na wizi na iwapo mtu fulani alionekana kuwa yu mwizi mtu huyo alizomewa sana na pia wanakijiji walimnyima mwizi huyu haki yake ya kuoa mke (Social Control). Kwa hiyo watu waliogopa kuiba ili wasije wakaambiwa ni wezi na kukosa mwanamke wa kuoa. Siku hizi wezi ni wengi mno hata wananchi huwa na wasiwasi sana katika kujenga ghala zao mbali na majumba yao. Sababu kubwa zinazofanya wizi uongezeke ni kwamba viongozi wengi wavijijini huogopa ku wafichua wezi na pia huhongwa pombe na wale ambao ni wezi.

Basi jamaa hawa hushindwa kutekeleza wajibu wao sawasawa. Wakati mwingine mwizi aweza kukamatwa na wanakijiji na kumpeleka mwizi huyo kwa bwana hakimu. Wanapofika huko naye, hao wanakijiji wanaulizwa maswali kama wanao ukweli kwamba mtu waliyemleta ni mwizi. Basi wanakijiji wengi hukata tamaa na mara nyingi wanakijiji wengine hujichukulia madaraka mikononi mwao na kumwadhibu yule mwizi vibaya sana.

Kuhama kwa watu[hariri | hariri chanzo]

Zamani watu walikuwa wachache sana na kuhamahama kwao kulikuwa kuchache. Kuhamahama kulitokea tu wakati njaa ilipoingia katika nchi fulani au vita kutokea, basi jamaa walihama. Kuhamahama kwa Wasafwa twaweza kusema kuwa walihama mara yao ya mwisho walipoingia nchi ya Usafwa miaka mingi iliyokwishapita. Shida zao zilikuwa ni hizo hapo juu zilizo wafanya watu wahamehame na kwa jumla kuhamahama kulisababishwa na maafa hayo. Siku hizi Wasafwa wengi, hasa vijana huhamia sehemu zile zilizo na nafasi ya kazi kama vile mji wa Dar es Salaam, sehemu zenye mikonge mingi - Tanga - Kilosa - Morogoro na kadhalika.

Pia Wasafwa wengi walio vijana wamehamia nchi za Zambia ambako kazi nyingi zapatikana katika migodi na viwanda. Wasafwa wazee ndio hubakia nyumbani kwa sababu ya jukumu walilo nalo juu ya familia zao, na pia wao hawapendi zaidi kuhamia nchi za kigeni ambazo zina watu walio na desturi na mila tofauti na za kwao. Zaidi na zaidi wazee wa Kisafwa hubakia nyumbani wakilima mashamba yao. Kundi lingine lililo na uhuru wa kuhamia sehemu zilizo na nafasi za kazi ni wale Wasafwa ambao hawajaoa.' Hawa huhamia sehemu zilizo na kazi bila taabu kwa sababu hawana matatizo ya familia. Lakini kwa jumla vijana wa Kisafwa wanaotaka kujaribu bahati yao katika maisha yao ndio wengi huhama kila mwaka.

Wanyama wafugwao[hariri | hariri chanzo]

Wasafwa si wafugaji hodari kama jamii zingine za Watanzania zilivyo. Wamasai, Wambulu, Wagogo, Wahehe, Wanyiha ni wafugaji wakubwa wa ng'ombe. Lakini Wasafwa walifuga wanyama wachache sana na mpaka sasa wanafuga wanyama wachache sana katika vijiji vyao. Walifuga mbuzi na ng'ombe wachache sana kwa ajili ya kutambika au kuwachinja wakati wa kilioni kwa ajili ya mboga, kwa wale waliopo kilioni. Siku hizi ng'ombe, mbuzi, kondoo, wanafugwa kwa ajili ya maziwa na nyama. Pia kuku na nguruwe wafugwa kwa sababu ya mayai na nyama.

Familia ya Kisafwa inaweza kuwa na baba mmoja, mama mmoja pamoja nawatoto, au inaweza kuwa na baba mmoja, mama wawili au watatu pamoja na watoto wao. Hapo zamani familia zilikaa katika vijiji kwa kufuata ukoo. Kwa hiyo kila kijiji kilikuwa na ukoo fulani.

Mtu alipoposa msichana basi alihamia katika kijiji cha msichana na kukaa huko na kuongeza jumla ya familia. Kwa hiyo familia iliyokuwa na mabinti wengi iliweza kupanuka sana na kufanya kijiji chao wao wenyewe cha wakwe na baba na mama mkwe na watoto na wajukuu, na kadhalika. Utaratibu huu wa kuishi pamoja namna hii kwa kufuata undugu bado unafuatwa na watu wengi katika nchi ya Usafwa. Jamii ya Wasafwa ni jamii inayofuata urithi kwa upande wa baba. Katika kurithi baba akifa ni lazima mtoto wa kwanza wa kiume arithi mali ya baba yake. Lakini katika kurithi mall ya baba, yampasa mtoto huyo aonyeshe busara safi, bila hivyo hawezi kurithi mali ya baba yake kwa sababu ya kukosa busara.

Mtoto wa pili aweza kuchaguliwa na ukoo wa baba ili aweze kurithi iwapo alionyesha busara safi, zaidi kuliko kaka yake mkubwa. Kwa kawaida warithi walitoka kwa mke mkubwa, na iwapo mke mkubwa alikosa kuzaa watoto wa kiume na akazaa watoto wa kike, basi mtoto wa kiume wa mke wa pili aliweza kurithi.

Mirathi iligawanywa kwa ndugu zake wote, lakini yeye mrithi alizidishiwa mirathi zaidi kwa sababu yeye ndiye aliyebadili nafasi ya baba yake na alipaswa kuwatunza ndugu zake sawa sawa kama baba yao alivyokuwa akiwatunza alipokuwa bado yu hai. Siku ya kurithi, pombe nyingi ilipikwa na kutengenezwa na chakula kwa wingi kilipikwa ill watu wale na kunywa na kufurahi sana.

Watu walicheza na kuimba nyimbo za furaha. Utaratibu huu wa kurithi mali ya baba bado unafuatwa na Wasafwa wengi ingawa yapo mabadiliko mengi.

Ndoa[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida mvulana aliweza kusikilizana na msichana anayetaka kumchumbia. Baada ya hapo, mvulana alikwenda kwa baba yake na kumwambia ya kwamba anamtaka binti ya fulani amchumbie. Basi babake aliweza kumwambia mzee mwenzie pale kijijini kuwa aende akamwambie baba ya binti kuwa wanamtaka kumchumbia binti yake. Iwapo mzee wa binti huyo anakubali ombi la wazee wenzie, basi posa inapelekwa.

Njia ya pili ya kumposa msichana ni kwamba mvulana na msichana wanakubaliana waoane. Baada ya kufanya hivyo, wanaamua wote wawili kutoroshana bila ya wazee kujua, isipokuwa wazee wanaambiwa baada ya kutoroshana hao vijana. Kwa kawaida msichana hutoroshwa na mvulana ambaye atakuwa mumewe wa maisha. Mvulana humpeleka msichana huyo aliyetoroshwa kwa baba yake mvulana. Mzee wa mvulana akishaona mambo yamefikia kiwango hicho, huondoka haraka kwenda kwa mzee pale kijijini na kumwomba aende mara moja kwa baba ya msichana aliyetoroshwa na kumwambia ya kuwa wanataka kumuoa binti yake na kwamba kwa sasa binti huyo wamemchukua tayari yuko nyumbani kwao hao jamaa. Basi baba ya binti hukubali na kuwaambia ya kuwa wakalete mahari.

Kwa kawaida mahari ilikuwa kuku au ng'ombe au mbuzi mmoja au jembe lapelekwa kama posa au mahari. Zamani mahari yalikuwa si mengi na tena yalikuwa hayadaiwi sana kama siku hizi iwapo mtu aliyehusika alikuwa hana chochote bali alitaka kuoa mwanamke.

Vijana wa Kisafwa walikuwa hawana taabu katika kuoa mke kwa sababu mahari yalikuwa rahisi sana. Lakini siku hizi mahari yamekuwa makubwa; Ng'ombe sita au zaidi hudaiwa kama mahari na hii yasababisha kushindwa kwa vijana wengi wa Kisafwa kuoa wanawake na wanawake kushindwa kuolewa. Kwa hiyo namba ya wanawake wasioolewa huzidi na ya wanaume yaongezeka, na mwishowe umalaya waongezeka nchini.

Kwa jinsi hii, ile mila ya zamani ya Wasafwa ya kuukataa umalaya kabisa katika nchi yao umeanza kupungua. Yasemekana ya kuwa mtindo huu wa kutoza mahari mengi sana umeigwa na Wasafwa toka kwa Wanyakyusa ambao wana desturi ya kutoza mahari mengi watoto wao wanapoolewa. Tabia hii ya kutoza mahari mengi ilianza kuigwa tangu mwaka 1919.

Baada ya mahari kupelekwa kwa baba ya msichana, basi yule kijana huanza kumsaidia kazi nyingi baba mkwe wake. Wakati mwingine aweza kulima shamba la mkwewe nyumbani kwake.

Iwapo watoto hawakutoroshana, basi baada ya posa kupelekwa kwa baba mkwe, wazazi wa msichana wanaweza kumleta binti yao kwa bwana yake wakati wowote ule na wala hakuna sherehe kubwa katika kufanya hivi. Baada ya ndoa, mvulana pamoja na msichana (mkewe) huhamia kwa baba mkwe na kujenga nyumba yao huko. Ilikuwani lazima msichana avunje ungo ndipo aweze kuposwa.

Inampasa mtoto wa kiume amsaidie baba wa msichana kama posa au mahari ilirudishwa kwa mwenyewe baadae kama alishazaa mara moja kwa baba mkwe. Mtamba alibakia kwa baba mkwe.

Ndoa ya siku hizi[hariri | hariri chanzo]

Mvulana baada ya kupatana na msichana anayetarajia kumwoa humpa msichana huyo shilingi ishirini, na msichana huchukua hizo shilingi ishirini na kununua nguo yoyote ile inayompendeza, bila ya kuwaeleza wazazi wake. Kama wazazi wake wakimwuliza kapata wapi nguo aliyovaa, huwaambia kauza kuni ndizo zilizomletea fedha za kununulia nguo. Baada ya hapo, mchumba wake aweza kumchukua mchumba wake bila ya wazazi wa msichana kujua na kumpeleka mchumba wake hadi kwa mama yake mvulana ambaye naye hutoa shilingi ishirini na kumpa huyo mchumba wa mtoto wake. Baada ya kufanya hivyo, habari zinaietwa kwa wazazi wa msichana kuwa mtoto wao wanaye nyumbani kwao na kwamba wanataka kumuoa. Wazazi wa msichana hukubali na baada ya siku nne hivi, msichana hurudishwa kwa wazazi wake. Siku ya kwanza ambayo msichana huchukuliwa na mchumba wake, anapofika mlangoni kwa nyumba ya mama ya mchumba lazima apewe shilingi 150/- na mchumba wake. Safari ya pili, msichana huyo huchukuliwa na mchumba wake baada ya kukaa kwao msichana miezi mitatu au sita, na sasa msichana hupelekwa moja kwa moja hadi nyumbani kwa mvulana, ambako hulala siku mbili hivi, halafu baba ya mvulana huwaambia wazazi wa msichana kuwa binti yao yuko hyumbani kwake. Wazazi wa msichana humwambia baba ya mvulana kuwa warudishiwe binti yao siku ya pill. Basi msichana hurudishwa saa za jioni siku hiyo ya pili na msichana hupewa shilingi tatu au nne hivi kama kuku wa kuwapa wazee wake ikiwa kama ni adhabu.

Msichana hukaa kwa wazazi wake kiasi cha miezi miwili au sita kwa kutegemea mahari aliyonayo mchumba wake. Kama mahari ipo, basi msichana hatakaa miezi mingi kwao bila kwenda kwa mchumba wake ambayo hupelekwa kidogo kidogo kwa wazazi wake.

Safari ya tatu, msichana huchukuliwa tena na mchumba wake na kupelekwa nyumbani kwa mchumba wake. Mpaka wakati huu msichana hawezi kupika chakula cha mume wake sababu bado hajawa ni mke. Wakati wote huu wanapata chakula chao toka kwa mama ya mvulana. Msichana hukaa siku mbili kwa mchumba wake na siku ya tatu baba ya mvulana hutoa habari kijijini kwao kuwa waanze kutayarisha pombe na vyakula vichache. Baada ya kuona kuwa pombe imekuwa tayari, baba wa msichana huwaambia wazazi wa mvulana ya kuwa wawarudishie binti yao. Wakati huu baba wa mvulana hujitayarisha sawa sawa na huvunja fedha kiasi cha shilingi mia nne ambazo huwa katika mahela mahela au vikoroti.

Siku hiyo wazazi wa msichana hunywa pombe sana na huwachagua wazee fulani ambao hutumwa kwa baba ya mvulana na kusema kuwa wanamtaka binti yao. Halafu baba wa mvulana humchagua mtu mmoja wa kumpeleka msichana kwa wazazi wake. Mtu huyo aneyempeleka msichana kwa wazazi wake ndiye anayeshika helazote hizi zilizovunjwa na mzazi wa mvulana, na pia jamaa huyu hufuatana na ndugu wa mvulana wakati wa kumpeleka msichana nyumbani kwao.

Msichana hutembeatembea kidogokidogo ili aweze kupewa fedha nyingi sana, na hujaribu kutafuta sababu nyingi na visingizio vingi ill aweze kusimama, na akisimama hupewa fedha ili aweze kutembea. Kwa njia hii msichana huyo aweza kuchuma fedha nyingi sana kiasi cha shilingi mia tatu au zaidi kabla hajafika nyumbani kwao. Wafikapo nyumbani kwa wazazi wa msichana, wale waliokuja kumsindikiza msichana hupewa pombe kiasi cha madebe thelathini hivi na kuyapeleka nyumbani kwa baba ya mvulana. Huko nyumbani kwa wazazi wa mvulana hunywa pombe waliyopewa na wazazi wa msichana. Lakini wazazi wengine wa mvulana wanaweza kutoa kila mmoja shilingi tatu halafu kila mmoja akichukua debe moja la pombe na kwenda nayo nyumbani kwake na kuinywa. Kila ndugu ya baba ya mvulana aweza kutoa shilingi tatu na kuchukua debe moja la pombe.

Msichana hulala siku moja nyumbani kwao. Baada ya siku hiyo, baba ya mvulana huenda nyumbani kwa wazazi wa msichana kwenda kumpa baba ya msichana shilingi kumi na tano. Katika safari hii, baba wa mvulana hufuatana na wenzie watatu au watano hivi. Baada ya kupokea zile shilingi kumi natano, baba wa msichana huwapa binti yake wazazi wa mvulana. Kesho yake, baada ya msichana kufika nyumbani kwa bwana yake, huanza kutayarisha mafiga na kupika chakula cha bwana yake kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya kuwa mwanamke aliyeolewa.

Bwana wake hawezi kula chakula hicho kilichopikwa na mke wake mpaka kwanza mke ampe bwana yake shilingi sitini ndipo ale chakula chake. Chakula kingine kilichopikwa na huyo mke kinapelekwa kwa baba mkwe. Mali kadhalika baba mkwe hawezi kula chakula cha mkwe wake mpaka naye apewe na huyo mkwe wake (mke wa mtoto wake) shilingi ishirini na tano ndipo ale chakula chake. Bila ya kupewa hizi shilingi ishirini na tano baba mkwe hawezi kula chakula cha mkwe wake.

Hizo shilingi ishirini na tano zatiwa pembeni mwa sahani za chakula wakati wa kupeleka chakula kwa baba mkwe.

Baada ya hapo, msichana huyo huendelea kuwapelekea chakula baba na mama ya bwana yake, mpaka watakapomkataza asiwapelekee chakula tena. Sasa atakuwa mwanamke kamili nyumbani.

Sifa za wachumba[hariri | hariri chanzo]

Wachumba wanatakiwa wawe na sifa nzuri kabla ya kuoana, yaani wanatakiwa wasiwe wezi au wasitoke katika ukoo wa watu walio wezi wasiwe malaya. Wanatakiwa wawe wema na wasiwe wachoyo bali wawe wakarimu. Inawabidi watoke kwenye koo zilizo nzuri na bora. Magonjwa kama ukoma yalitiliwa mashaka makubwa katika posa. Iwapo mchumba mmojawapo anatoka katika ukoo ulio na ugonjwa wa ukoma basi mchumba huyo itamwia vigumu sana kumpata mchumba mwenzie.

Kwa kawaida mkoma hutengwa mbali sana na watu wengine na kujengewa nyumba yake ya pekee chini ya mti wa mlagalila, na anapokufa mkoma huzikwa chini ya huo huo mti halafu mti wenyewe hukatwa ili uangukie nyumba yake na vyombo vyake vyote vifunikwe kabisa. Makusudi ya kufanya hivi ni kwamba Wasafwa wanajaribu sana kuepusha watu wasio na ugonjwa huu wasikamatwe nao.

Walakini sifa zote hizi zilizoelezwa hapo juu kuhusu wachumbazimeanza kusahauliwa, na sasa watu wengi wa Usafwa hawaangalii sana sifa hizi kwa sababu ya elimu nyingi na pia mwingiliano wa utamaduni mbali mbali wa kigeni.

Sherehe haikuwa kubwa sana bali kitu kikubwa sana katika ndoa yao kilikuwa kudumisha ndoa yao kwa wale waliohusika. Ndoa za Kisafwa zilidumu sana bila kuvunjika, lakini siku hizi ndoa nyingi zinazofungwa hazidumu sana kwa sababu ya mabadiliko ya maendeleo yaliyokwisha tokea yakiambatana na utamaduni wa kigeni. Ingawa kuna sherehe kubwa zinazofanyika siku hizi wakati wa arusi, lakini ndoa nyingi hazidumu sana kama zamani. Ingawa kuna mabadiliko mengi ya utamaduni katika jamii ya Wasafwa lakini Wasafwa ni watu ambao hawakupoteza sana utamaduni wao kama jamii zingine za mkoa wa Mbeya zilivyopoteza utamaduni wao.

Kila msichana alipimwa bikira yake kabla ya kupelekwa kwa bwana yake. Hii ilikuwa ni desturi ya jamii nyingi za Mkoa wa Mbeya. Kwa kawaida wasichana wote wa Kisafwa walitunza bikira zao vizuri sana mpaka siku ya kuolewa. Lakini siku hizi nidhamu hii imeanza kupungua uzito wake kwa sababu ya mwingiliano wa ustaarabu mbali mbali.

Talaka[hariri | hariri chanzo]

Hapo zamani talaka katika jamii ya Kisafwa zilikuwa nadra sana kupatikana. Mwanamke kutoka kwa bwana yake na kwenda kwa bwana mwingine ilikuwa shida. Pia bibi kumtoroka bwana na kutorokea kwa bwana mwingine ilikuwa vigumu sana. Iwapo mwanamke alifanikiwa kufanya hivyo, vita kati ya kijiji alikotoka na kijiji anakotorokea ilizuka. Ng'ombe na wanawake wa kijiji alikotorokea walitekwa kwa hiyo kumtorosha mke wa mtu au kumghilibu akili zake, watu waliogopa sana matokeo yake. Kwa hiyo upuuzi huu wa kutoroshana au kumtaliki mwanamke ovyo ulikuwa nadra sana. Kwa hiyo vita ilipiganwa na kusababisha hasara kubwa kwa pande zote, hasa kwa wanakijiji waliommvua iweze kunyesha. Mfano wa sehemu mojawapo zilizo maarufu sana kuomba (kutambikia) mvua ni Iganjo, sehemu za Uyole karibu na mlima Mbeya. Kwa kawaida chifu wa jadi, ambaye watu wa sehemu hizo humwita Mfalme, huwa ndio kasisi Mkuu wa matambiko, lakini sehemu zingine za Usafwa Mzee fulani anayeaminika na kufuatana na chifu wao, ndiye huwa Kasisi Mkuu wa kuomba mvua. Yeye hutafuta ulezi wa kukorogea pombe na baada ya pombe hii kukorogwa na kuwa tayari pombe hiyo yatiwa ndani ya vibuyu vitano au sita. Kisha kasisi huwatangazia wazee wanaohusika na salaza kuombea mvua na sifku huchaguliwa ili kufanya shughuli zote hizi.

Sasa kuku mweusi hutafutwa (sehemu zingine mbuzi au kondoo hutafutwa kwaajili ya shughuli hizi). Mambo yote yakiwa tayari watu wote wanaohusika hjuenda mahali palipo patakatifu na kuanza kuomba mvua inyeshe. Kasisi mkuu huanza kusema maneno haya. "Uposhele inguku ini tuhanzaje hwunzi hwilwipei invula itonye, iviyabo vihwone. Ingukuinj mulyarrje mwendi mwikwizyanajei abantu balalamiha baiga, "Tukosile yenu? Invulayinyu Mhutima?"Tulaba twalamba sana ngatukosile shimo vyanje. Ngazilipo zimo uvitilwe utuwozye we wewe dada pipo nahumo uhwinyi washimbilile. Tusubila wenewe ungulubi uwinji numo."

Maana yake: "Pokea kuku huyu tunataka nchini kuwe kweupe, Mvua inyeshe vyakuia vinakauka. Watu wanalalamika wanasema,Tumekosa nini? Kwa nini unatunyima mvua? Tunakuomba sana kama tumekosa lolote useme. Kama kuna jambo lolote lililokukasirisha utuambie wewe baba. Kwa sababu hakuna mahali pengine pa kukimbilia. Tunakutegemea wewe mwenyewe, Mungu mwingine hakuna."

Wakati sala hizi zinaposemwa, pombe iliyo katika vibuyu viwili yamwagwa chini mahali patakatifu na huku kuku atiwa ndani ya pombe iliyomwagwa chini na hushikiliwa hivyo hivyo mpaka kuku huyu kukosa hewa kabisa na kufa kwa kushindwa kuvuta hewa.

Baada ya kuku kufa manyoya yake yananyonyolewa na nyama yake huchomwa. Baada ya kumchoma kuku huyo, kasisi huchukua nyama kidogo na maini yake na kukata kata vipande vidogo vidogo vya nyama ambavyo vyatiwa pembeni mwa mahali pale pombe imemwagwa. Nyama inayobaki inaliwa na makasisi wadogo waliopo hapo pamoja na kasisi Mkuu, Makasisi hao wadogo huwa watano au kumi hivi kwa kutegemea na mahali penyewe na watu walivyo na shida zao, na jinsi wanavyotaka kuomba mvua yenyewe. Lakini kabla ya kusema sala zao, wale makasisi, wengine hucheza cheza kwanza hapohapo mahali patakatifu isipokuwa kasisi mkuu na kusema, "Tumefika sisi watoto wenu msije mkasema ni watoto wengine". Ndipo kasisi mkuu huwaambia makasisi wake wakae chini halafu huendelea na sala kama ilivyoelezwa hapo juu na mvua hunyesha mara baada ya sala hizo.

Wakati mahindi yamekomaa mashambani hakuna mtu wa kuanza kuvunja mahindi hayo kutoka shambani mwake na kuanza kula mpaka kwanza sherehe maalum imefanyika. Sherehe ya namna hii hufanyika sehemu zingine zingine katika nchi ya Usafwa. Mwezi wa tatu ambapo ndiyo wakati mahindi yaanza kukomaa kiasi cha kuweza kuliwa, Kasisi mkuu huwakusanya watu wote wa sehemu yake na kuwaambia siku ya kukutana pamoja kwa ajili ya shughuli ya ufunguzi rasmi wa kuanza kula mahindi mapya. Siku hiyo ikifika watu wote huondoka na kwenda mahali pa kukusanyikiana huku wakichukua mapembe na fimbo na miilini mwao na usoni hujipamba kwa rangi mbali mbaii. Siku hiyo wanakijiji hao hucheza sana kuanzia saa saba adhuhuri hadi saa moja jioni.

Wakati wa kucheza, watu huwa katika safu - wanaume upande mmoja na wanawake upande mwingine, na wale walio na mapembe hufanya safu, ya katikati. Wakati wa kucheza watu hawavai mavazi rasmi balil huvaa mavazi ya kawaida tu. Kasisi Mkuu huvaa shuka na kaptura hukamata mikuki mitatu, halafu hupanda juu ya mti na huko mtini huchomeka mikuki miwili. Baada ya kufanya hivyo, kasisi hushuka chini na mkuki mmoja. Saa za jioni huwakusanya watu wote halafu humwaga unga wa malezi chini na kusema.

"Baba Inshinshi tuongene apa usanyono, Tuhwanza aje iviyabo vimelaye ishinza mwatulima Idondoma tumanyile aje linanganya, Tulawa ugazije amalondoma gasinanganaye iviyabo Nantele baba pahandinealine amagonda gao, Iviyabo vyao vyamelile ishi bahwande aje balyanje. Ovisaye abantu basinanganye, Tumanyile aje balipo abitunga, Tulaba aje ngoshele balipo abitunga bawoneshe, Utuvuzye aje abitunga babana nganya, balipo abantu bafumu nutali,

Wakati wa kutawazwa, huyo Mundewa au chifu hukalishwa juu ya kigoda huku amefunikwa nguo. Shughuli hii hufanywa na mtani - ndiye kasisi wa sherehe zote hizi. Halafu Mundewa huvikwa kikomo mkononi. Baada ya hapo huyo jamaa anayetawazwa hupewa shoka, mundu, zana za kufyekea miti na majani shambani. Mkuki - alama ya kuonyesha iwapo vita itatokea aweze kulinda Taifa lake. Akiwa bado kigodani, mfalme huyo hutemewa pombe kinywani mwake toka kinywani mwa mtani anayefanya kazi ya kumtawaza siku hiyo na anaimeza pombe hiyo.

Mfalme huyo hula kiapo cha kutawala nchi kama hivi: Uleke ukobo - acha kuwanyima watu. Uleke ugoni ugoni - acha mambo ya uzinifu. Uleke upekeupeke - acha uwongo.

Wewe jina lako liwe "Nifenazo" - yaani "Wewe uwe mtunza siri, cheka na kila mtu". "Mhasemwe wadala" - usisahau wazee. Halafu mfalme anatiwa mafuta ya nyonyo kichwani pake, halafu mafuta yale hutiririka kuja usoni - puani mpaka mdomoni; halafu mtani wake wa kike huja na kuyalamba mafuta yale yaliyotiririka karibu na mdomo wa mfalme na kuyameza.

Mtani anayefanya kazi hii ya kumtawaza mfalme hupewa mbuzi kama zawadi yake kwa kazi aliyoifanya siku hiyo. Halafu huyo mtani huingia ndani ya nyumba ya mfalme na kulala juu ya kitanda cha mfalme na kumwita mke wake mtani na kulala naye juu ya hicho kitanda cha mfalme ila hawatendi jambo lolote. Nyumba ya mfalme hunyunyiziwa hoza ill kuipooza.

Maji ya kunywa ilikuwa lazima yatoke kisimani ambacho kilichimbwa katika kila kijiji cha Wasagara - hasa kisima kilichimbwa chini ya mti mbali kidogo na kijiji kuhakikisha kuwa maji hayakuchafuliwa na chochote. Maji ya mto Mkondoa hayakutumika kwa kunywa ila kwa kumwagilia mashamba tu. Kisima chenyewe kilifunikwa na magome ya miti. Maji ya kufulia nguo na kuoga yalitoka kisimani, na yalitekwa na kutiwa katika chungu kikubwa kilichotengenezwa kilichoitwa "Ponda".

Wasagara walikuwa wanatengeneza mavazi ya wao wenyewe kabla ya kuletwa mavazi mapya na wakoloni. Walitengeneza mavazi yao toka kwenye magome ya miti ya "Mlenye". Gome la mti huu liliondolewa vizuri sana kwa kutumia shoka na tezo, halafu likalainishwa vizuri sana kwa kulipon-daponda na jiwe au kipande cha mti na kisha likavaliwa kiunoni. Kofia vile vile zilitengenezwa kutokana na magome ya miti hii ya "Mlenye".

Mbeleko ya kubebea mtoto na viatu vyote vilitengenezwa kutokana na hayo hayo magome ya miti. Wakati mwingine viatu vilitengenezwa kutokana na ngozi ya mbuzi.

Mwanamke alijipaka mafuta ya nyonyo ambazo zilikuwa zikipandwa sana wakati huo na ambazo mpaka wakati huu zapandwa sana kama zao la kuwaletea fedha. Masikio ya wanawake yalitobolewa na kutiwa mpingo. Nywele zao zilikatwa halafu zikatiwa mafuta.

Mila na desturi za Wasagara ni kwamba watu hawa wana asili ya kushirikiana sana katika shughuli za kuzalisha mali karibu kila kazi walioifanya walishirikiana pamoja kama kijiji na kazi zao za kulima mashamba ziliisha mara moja kabla ya mvua kunyesha. Mkuu wa kijiji, baada ya kusikia ngurumo ya mvua alipiga mbiu ya mgambo na kuwatahadharisha wanakijiji wote kuanza kulima mashamba yao. Na kazi hii walifanya kwa zamu hata ikatokea kwamba mashamba yao mengi yalilimwa mapema. Umoja ni nguvu na Utengano ni udhaifu. Kuna haja kubwa ya kufufua desturi hii ya kufanya kazi pamoja ili wananchi waweze kushirikiana kama zamani katika kutekeleza kazi zao barabara na upesi zaidi.

Zaidi ya hayo, zamani Wasagara walikuwa hawana shida yachakula-yaani chakula kilipatikana kwa urahisi wakati wo wote wa kiangazi au wa masika.

Wasagara walilima na kupanda mazao ya chakula mara mbili kwa mwaka. Wakati wa masika mimea yao mashambani ilitumia maji ya mvua na wakati wa kiangazi mimea yao ilitumia maji ya kumwagilia ya mto Mkondoa. Mboga nyingi za majani zilipandwa wakati huu kwa kutumia maji ya mto lakini jambo hiii sasa halifanyiki hata kidogo kwa sababu utaalamu ule wa zamani umepotea na pia mto wa Mkondoa sasa uko chini kidogo kuliko ilivyokuwa hapo zamani. Manufaa yote ya kutumia maji ya kumwagilia ya mto Mkondoa kwa kumwagilia mashamba hamna sasa isipokuwa mto huu unatumika tu kwa kuogelea, kufulia na kuvua samaki.

Mto wenyewe haukauki na tena ni mkubwa, kwa hiyo ingalikuwa vyema zaidi kama mifereji midogo midogo ingalitengenezwa ili ipeleke maji katika mashamba au bustani wakati wa kiangazi.

Na wakati wa masika mifereji hii ingaliweza kuzibwa kwa sababu wakati huu hakuna haja ya kutumia maji ya mto wakati ipo mvua. Isipokuwa kama mvua imeshindwa kunyesha. Kitendo hiki kingekuwa cha manufaa sana kwa Taifa zima kwa kutumia utaalamu wa kisasa.

Jambo jingine la kulifufua ni ulinzi wa Taifa.

Wasagara walikuwa na ulinzi mkubwa wa vijiji vyao kila mwananchi alikuwa najukumu hilo. Tukifanya Kama walivyolinda Taifa lao hawa jamaa tutaweza kwenda mbali zaidi katika kulilinda Taifa la Watanzania lisiingiliwe na maadui wowote.

Katika kufanya kazi, kila mtu katika nchi ya Wasagara alikuwa na wajibu wa kufanya kazi, kila mtu alipewa kazi ya kufanya na jamii. Mvivu aliadhibiwa na kuzomewa na pia alipewa kazi ya kufanya kwa kupimiwa ngwe yake Mwenyewe ili aimalize Mgonjwa na mtoto ndio hawakupewa kazi kwa sababu walikuwa hawajiwezi. Lakini mtu mzima yeyote mwanamke kwa mwanaume, wote walifanya kazi pamoja bila kutegeana. Desturi hii ilikuwa nzuri sana kwa maoni yangu naona kama ingalifufuliwa na kuenezwa kila mahali nchini ili kila mtu awe na kazi ya kufanya.

Heshima na adabu vilitiliwa mkazo sana katika jamii ya Wasagara, hasa heshima kwa wakubwa na viongozi wa Wasagara. Huu ni mfano wa kuiga sana toka kwa watu hao. Heshima na adabu kwa viongozi wetu ni wajibu wetu. Ni lazima tuwape heshima wanaostahili kupewa na walio chini yao. Kwa sababu vijana wengi wameanza kupoteza heshima na adabu kwa viongozi wetu, ingalifaa kama jambo hili lingefufuliwa upesi sana kwa sababu heshima hainunuliwi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Wizara ya Utamaduni : Historia fupi ya Utamaduni wa Mtanzania. 1974.
  • CharsleyS.R.: The Princes of Nyakyusa, 1969.
  • Mwakipesile J.S.: Utamaduni wa Wasagara, 1974.
  • A.M.T. Mabeleand Bjarne F.K. Gorm P.. Strategies and methods of the

Development of museal Activities on local Level in Tanzania; 1974.

  • MwakipesileJ.S.: Jamii ya Wasafwa, 1974.
  • Dr. S.A. Lucas & A. F. Masao: The Present State of Research on cultural

Development in Tanzania, 1974.

  • Dr. I.K. Katokeand Dr. S.A. Lucas: Cultural Development as a factor in social charge, 1975.