Waraka wa pili wa Klementi
Waraka wa pili wa Klementi ni andiko la Kigiriki karne ya 2 lililopewa jina la Papa Klementi I[1] ambalo ni kati ya yale ya kwanza ya Ukristo nje ya Biblia (Agano Jipya) yaliyohifadhiwa na kujulikana hadi leo. Pengine liliingizwa pamoja na waraka wa kwanza wa Klementi katika matoleo ya Biblia ya Kikristo, lakini baadaye liliachwa nje tena wengi walikanusha kuwa kazi ya Papa huyo[2], kuanzia Eusebi wa Kaisarea[3] na Jeromu[4].
Vilevile inaonekana kuwa si barua kwa Wakorintho kama ilivyodhaniwa awali[5], bali hotuba[6] ya miaka 120-140 BK.
Iliandikwa kwa lugha ya Kigiriki, iliyokuwa inatumiwa na Wakristo wengi wa wakati ule hata mjini Roma.
Pamoja na maandiko mengine kama vile Didake, Waraka wa Barnaba na nyaraka saba za Ignas wa Antiokia iko kati ya Mababu wa Kitume, yaani maandiko ya kale kabisa ya Ukristo yaliyohifadhiwa nje ya Agano Jipya.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Brannan, Rick (2017). The Apostolic Fathers: A New Translation. Lexham Press. uk. 3. ISBN 978-1-68359-064-4.
- ↑ Holmes 2007, Second Clement
- ↑ Eusebius Pamphilius 325, Book3, Chapter 38
- ↑ Jerome, De Viris Illustribus, Chapter 15
- ↑ Petersen 2006, p. 392
- ↑ Donfried 1973, p. 487
Vyanzo
[hariri | hariri chanzo]- Donfried, Karl (Oktoba 1973), "The Theology of Second Clement", The Harvard Theological Review, 66 (4), Cambridge University Press: 487–501, doi:10.1017/S0017816000018149, ISSN 0017-8160, JSTOR 1509081, S2CID 170816578
{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - Eusebius Pamphilius (325), Ecclesiastical history (PDF), iliwekwa mnamo 2012-11-27
- Holmes, Michael (1 Novemba 2007), Apostolic Fathers, The: Greek Texts and English Translations, Grand Rapids: Baker Academic, ISBN 978-0-8010-3468-8, iliwekwa mnamo 2012-11-27
{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - Petersen, William (Novemba 2006), "Patristic Biblical Quotations and Method: Four Changes to Lightfoot's Edition of "Second Clement"", Vigiliae Christianae, 60 (4), Brill: 389–419, doi:10.1163/157007206778926292, ISSN 0042-6032, JSTOR 20474780
{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Marejeo mengine
[hariri | hariri chanzo]- Tuckett, Christopher M. (2012). 2 Clement: Introduction, Text, and Commentary. Oxford University Press. ISBN 978-0-19-969460-0.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- An extensive list of English translations of 2 Clement
- Chapters 1 to 10 in Greek[usurped]
- Chaapters 11 to 20 in Greek[usurped]
| Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa pili wa Klementi kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |