Wang's Family

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wang's Family ni tamthilia ya Kikorea inayohusu familia yenye watoto watano: wanne wa kike na mmoja wa kiume. Katika tamthilia hii kuna mafunzo tofauti ya kifamilia yanayofanywa. Mafunzo haya hutolewa kupitia maisha ambayo watoto hawa watano hupitia. Familia hii ni familia ya Wang.

Mtoto wa kwanza wa familia hii anaitwa Subac. Binti huyu ni binti aliyependwa sana na mama yake kuliko wanae wote. Binti huyu aliweza kubahatika kuwa na elimu zaidi ya wadogo zake na hata akaolewa na mwanamume aitwae Ming Jung aliye na pesa na makampuni. Lakini siku siyo nyingi baada ya kupata watoto wawili makampuni ya kijana Ming Jung yanafilisika, kitu kilichosababisha upendo kati ya mama Subac kupungua na kuilazimu familia nzima ya Subac kuhamia katika nyumba ya mama Subac kwa kuuza nyumba pamoja na samani zao zote. Huu unakuwa muda mgumu sana kwa Ming Jung kwa ajili ya kukabiliana na umaskini na kazi yake mpya ya kutoa huduma ya vifurushi nakurudi nyumbani amechelewa. lakini katika wakati huu Subac yuko akiangaika kununua vipodozi na kutumia vibaya pesa yao ya matumizi.

Video-x-generic.svg Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wang's Family kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.