Walter Mzengi
Walter Mzengi ambaye anajulikana pia kama Walt Mzengi Corey ni mwandishi, mkurugenzi na mwigizaji wa sinema, ni mzaliwa wa Tanzania anayeishi kati ya Dar es Salaam na New York City. Ni mmoja wa washindi sita bora wa shindano la filamu fupi lililoandaliwa na Netflix, huduma ya utiririshaji duniani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Walt Mzengi Corey hakuanza kazi yake katika utengenezaji wa filamu alianza kufanya kazi kama afisa masoko katika Pizza hut Tanzania. Bila kufahamu kuwa jaribio lake la kwanza la utengenezaji wa filamu lingemshawishi kuitazama kama taaluma, alianza kujirekodi pamoja na marafiki zake mchezo wa kuteleza kwenye barafu. Katika kipindi alichokuwa akifanya kazi ya uuzaji katika Pizza hut, Siku moja akiwa kwenye meza yake aliwaza kwamba kile anachofanya sicho alichoitiwa akathubutu kupitia matamanio yake ya utengenezaji wa filamu na kuona jinsi inavyofanya kazi kwake.[1]
Taaluma yake ya Utengezaji wa Filamu
[hariri | hariri chanzo]Walt Mzengi Corey aliamua kutafuta maarifa zaidi juu ya utengenezaji wa filamu, hii ilimfanya atume maombi kwa vyuo vikuu viwili 'AFDA' na Chuo Kikuu cha Cape Town (ACT) ambavyo vyote viko Cape Town, Afrika Kusini akapata bahati ya kukubaliwa na AFDA.[1]
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Walter Mzengi Corey alimaliza masomo yake ya chuo kikuu nchini Africa kusini. Mnamo 2022, alichaguliwa kama mmoja wa watengenezaji filamu sita walioshinda katika shindano la "African Folktales, Reimagined" na Netflix na UNESCO, na kusababisha kuundwa kwa Katope (2023), ambayo ilikuwa na onyesho la kwanza la ulimwengu katika Tamasha la Filamu fupi la Kimataifa la Clermont-Ferrand.[2] Mnamo 2024, Walt alialikwa kushiriki katika jopo la Siku ya Kiswahili Duniani katika Baraza la ECOSOC katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, ambapo aliwakilisha jumuiya ya filamu ya Tanzania kama mzungumzaji. Ameandika na kuelekeza filamu ambazo zimechaguliwa kwa tamasha kama vile Tamasha la Filamu la BlackStar na Ghuba (2019), na Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar akiwa na Timela (2021) na Katope (2023), ambalo lilishinda Tuzo la kifahari la Ousmane Sembène.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 "Tanzanian filmmaker emerges winner of Netflix competition". The Citizen (kwa Kiingereza). 2022-03-15. Iliwekwa mnamo 2025-08-11.
- ↑ "Waandaji filamu Kenya, Tanzania na Uganda ni miongoni mwa washindi wa awali wa shindano la UNESCO na Netflix | Habari za UN". news.un.org. 2022-02-01. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-12-16. Iliwekwa mnamo 2025-08-11.