Wafiadini wa Gorkum
Jump to navigation
Jump to search

Wakristo 19 maarufu kama Wafiadini wa Gorkum
Wafiadini wa Gorkum (walifariki Brielle, Uholanzi, 9 Julai 1572, ni Wakristo 19 wanaoheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu wafiadini kwa kuwa waliuawa na Waprotestanti kwa kukataa kujiunga nao na kujitenga na Papa.
Baadhi yao ni:
- Petro wa Assche
- Wilehadi wa Denmark
- Teodoriko van der Eem
- Nikasi wa Heeze
- Antoni wa Hoornaert
- Godefrid wa Melveren
- Nikola Pieck
- Fransisko wa Roye
- Antoni wa Weert
- Jeromu wa Weert
- Korneli wa Wijk-bij-Durstede
Wengi walikuwa Wafransisko.
Kwanza walitangazwa na Papa Klement X kuwa wenye heri tarehe 24 Novemba 1675, halafu watakatifu na Papa Pius IX tarehe 29 Juni 1867.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai[1].
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |