Nenda kwa yaliyomo

Wabozo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wabozo

Binti wa Kibozo huko mjini Bamako, Mali.
Idadi ya watu
132,100
Maeneo penye idadi kubwa kiasi
Lugha

Kibozo, Kifaransa

Dini

Uislamu

Wabozo (Kibambara: ߓߏ߬ߛߏ, kwa mwandiko wa Kirumi: Boso)[1] ni kundi la watu wa Kimande linalopatikana hasa kandokando ya Mto Niger nchini Mali.

Jina la Wabozo linadhaniwa kutoka katika neno la Kibambara ߓߐ߬ ߛߏ bɔ-so, linalomaanisha "nyumba ya mianzi". Ingawa watu wa jamii hii wanakubali jina hilo kwa kundi lote la kabila, wao wenyewe hutumia majina mahususi ya koo kama Sorogoye, Hain, na Tieye. Wabozo wanajulikana sana kwa uvuvi wao na mara nyingine huitwa "mabwana wa mto".

Lugha ya Kibozo, ambayo ni sehemu ya tawi la Kisoninke-Bozo la Kaskazini Magharibi mwa Mande, kwa muda mrefu imechukuliwa kama lahaja za lugha moja, ingawa kuna lahaja nne tofauti.

Vipengele vya utamaduni wa Kibozo vilichukua sura wakati wa Dola ya Ghana katika karne ya 10, ambapo Wabozo walichukua maeneo ya ukingo wa Mto Niger. Wao ndio waasisi wa miji ya Mali kama Djenné na Mopti.

Ingawa Wabozo ni Waislamu kwa kiasi kikubwa, bado wanadumisha desturi kadhaa za kiimani za jadi. Mnyama wao wa totemu ni fahali, ambaye mwili wake unawakilisha Mto Niger, huku pembe zake zikiwakilisha pirogi (mitumbwi) za uvuvi za Kibozo.

Sensa ya mwaka 2000 ilihesabu idadi ya Bozo nchini Mali kuwa 132,100.

Bibliografia

[hariri | hariri chanzo]
  • Ligers, Ziedonis (1964–1969). Les Sorko (Bozo), maîtres du Niger: étude ethnographique (four volumes). Paris: Librairie des Cinq Continents.
  • in ISBN 3-570-19230-X: Geo Special Westafrika, Article: Sexualkunde am Fluss

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wabozo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.