Wabariba
Wabariba (wanaojiita Baatonu; wengi: Baatombu) ndio wakazi wakuu wa wilaya za Borgou na Alibori, Benin, na ni waanzilishi wa ufalme wa Borgu katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Benin na magharibi-kati mwa Nigeria. Nchini Nigeria, wanaishi katika Jimbo la Kwara magharibi na sehemu ya Borgu ya Jimbo la Niger. Kuna labda watu milioni moja wa Bariba, 70% yao wakiwa nchini Benin, ambapo ni kundi la etnia la nne kwa ukubwa na wanachukua karibu 1/11 ya idadi ya watu (9.2%).
Watu wa Bariba wamejikita hasa katika kaskazini-mashariki mwa nchi, haswa karibu na mji wa Nikki, ambao unachukuliwa kuwa mji mkuu wa jadi wa Bariba. Mwishoni mwa karne ya 18, walijitenga na kabila la Yoruba wa Oyo na wakajenga falme kadhaa katika eneo la Borgou. Ukoloni wa Benin (wakati huo Dahomey) na Wafaransa mwishoni mwa karne ya 19, na kuanzishwa kwa mpaka wa bandia wa Kiingereza-Kifaransa, ulimaliza biashara ya Bariba katika eneo hilo.
Moja ya sherehe zao maarufu ni sherehe ya mwaka ya Gani ambapo kuendesha farasi ni sehemu muhimu
. Watu wa Bariba wana nafasi muhimu katika historia ya nchi. Katika karne ya 19, Bariba walijulikana kuwa na madola huru na kutawala katika miji kama Nikki na Kandi kaskazini-mashariki mwa nchi. Katika mji wa Pehunko, kuna takriban watu 200,000 wa Bariba kati ya wakazi 365,000.
Kilimo ndio shughuli kuu ya watu wa Bariba. Wanapanda mahindi, mtama, mpunga, pamba, muhogo, viazi vitamu, maharage, mafuta ya mawese, karanga, na pia wanafuga ndege na mifugo. Dini inachukua nafasi muhumu kwa kabila la Bariba na kwa kiasi kikubwa ni Waislamu. vilevile, jamii kadhaa za Bariba zina imani za asili zao.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wabariba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |