Waarabu wa Tanzania

Waarabu wa Tanzania ni kundi kubwa la wakazi lililo na mizizi mirefu nchini, hasa katika maeneo ya pwani na funguvisiwa la Zanzibar. Waliohamia wanakadiriwa kuwa 70,000 hivi[1], lakini wenye asili ya Uarabuni wanaweza kufikia 493,000. Kihistoria Waarabu walijulikana kama wafanyabiashara na makabaila, lakini siku hizi wengi wanajihusisha na ujasiriamali, uvuvi na kilimo. Wengi wanaongea vizuri Kiswahili, lugha yenye athari kubwa ya Kiarabu. Wengi wanasema pia "Kiarabu cha Pwani" au wanatumia Kiarabu kwa ajili ya ibada.
Upande wa dini, karibu wote ni Waislamu Wasuni, ingawa wapo pia wachache Waibadi na Washia.

Historia
[hariri | hariri chanzo]Waarabu kutoka Omani, Yemen, na Uajemi walianza kuishi mwambaoni mwa Afrika Mashariki tangu karne ya 8, wakileta dini ya Uislamu na utamaduni wa biashara, ikiwemo biashara ya watumwa kupitia bahari ya Hindi.
Katika karne ya 19, Sultan Seyyid Said alihamisha makao makuu kutoka Muskat, Omani, hadi Zanzibar, akiunda utawala wa kikabila uliotegemea biashara ya viungo na ya watumwa.
Muda mfupi baada ya uhuru, Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yalisababisha maelfu ya Waarabu kuuawa na wengine wengi kukimbia nchi.
Zanzibar, hasa Mji Mkongwe, inabaki kiini cha ustaarabu wa Kiarabu nchini, lakini jumuia nyingine za maana zinapatikana pia Dar es Salaam (kwa namna ya pekee Upanga na Kisutu) na miji mingine ya pwani kama Tanga.
Athari yao
[hariri | hariri chanzo]Athari ya Kiarabu inaonekana wazi kotekote katika jamii ya Tanzania, hasa katika:
- Usanifu majengo, kama yale ya matumbawe yenye milango iliyochongwa.
- Mapishi, kama matumizi ya viungo (karafuu, bizari na mdalasini) na vyakula (pilau na biriani).
- Mavazi, kama kanzu na kofia maalumu (baraghashia) kwa wanaume na baibui au hijabu kwa wanawake.
- Muziki, kama mtindo wa Taarab, unaochanganya vipengele vya Kiafrika, Kiarabu na Kihindi.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Tanzania History and Information – Safari Info for Tanzania". eyesonafrica.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waarabu wa Tanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |