Waamadei

Waamadei walikuwa tawi la utawa wa Ndugu Wadogo lililotokana na juhudi za kuleta urekebisho za Amedeo da Silva (1420-1482). Ndiyo sababu waliitwa hivyo.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuanza mwaka 1464 katika konventi waliyopewa na mkuu wa shirika[1], mwaka 1568 waliungana na Waoservanti na kuenea katika konventi nyingine hata kuunda kanda ya kwao.
Kutokana na malalamiko ya walioogopa mafarakano shirikani, Papa Paulo II, kwa hati Inter caetera desiderabilia ya tarehe 22 Mei 1470, alifuta tawi hilo.[1] Lakini mwandamizi wake, papa Sisto IV alimuita Amedeo Roma, akampa konventi mjini akawakubali tena kwa hati Pastoris aeterni ya tarehe 24 Machi 1472.[1]
Papa Leo X kwa hati Ite et vos ya tarehe 29 Mei 1517, aliwaunganisha na Waoservanti: hata hivyo konventi zao zilibaki na uhuru fulani hadi tarehe 23 Januari 1568, ambapo papa Pius V, kwa hati Beati Christi salvatoris, aliziweka moja kwa moja chini ya watumishi wa kanda wa Waoservanti.[2]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Guerrino Pelliccia e Giancarlo Rocca (curr.), Dizionario degli Istituti di Perfezione (DIP), 10 voll., Edizioni paoline, Milano 1974-2003. (Kiitalia)
| Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waamadei kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |