Nenda kwa yaliyomo

Vyama vya Kiswahili Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muundo au mpangilio wa makala hii hailingani na masharti ya makala ya wikipedia. Inahitaji kuangaliwa upya.

Angalia mpangilio wa maandishi yake, umbo la vichwa na viungo ndani yake. Isipopangiliwa upya makala inaweza kufutwa.


Angalia ukurasa wa majadiliano! (Kibonye cha pili hapo juu kwenye dirisha hili)

Vyama vya Kiswahili Tanzania ni vingi. Kuna vilivyosajiliwa na ambavyo havijasajili. Bado haijulikani kama utiriri wa vyama vya lugha ya Kiswahili una hasara au faida zaidi.

Baadhi ya Vyama vya Kiswahili Tanzania

[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya vyama maarufu nchini Tanzania ni: Chama cha Lugha na Fasishi ya Kiswahili Tanzania (CHALUFAKITA), Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), Watetezii wa Kiswahili Tanzania (WAKITA), na Koja la Walumbi. Vingine ni CHAKAMA, CHAWAKITA, Linguistic Circle, na LAEA. Baadhi ya vyama hivyo vina tovuti zinazoeleza malengo na shuguli zake, CHAUKIDU. Vilevile, kuna taasisi na idara mbalimbali za Kiswahili katika vyo vikuu kadhaa nchini Tanzania kama vile Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Idara ya Lugha na Stadi za Mawasilino Chuo Kikuu Mzumbe. Pia, kuna mabaraza mawili ya kiserikali yenye dhamana ya kusimamia Kiswahili: Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA).

Pia, Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili Tanzania kimeanzisha Jarida la CHALUKITA mbalo limesajiliwa katika jukwaa la AJOL; jarida hilo lina umuhimu mkubwa sana katika ustawi wa Kiswahili kwa sababu linachapisha makala za kitaaluma za Kiswahili kila mwaka mara moja.

Je, Vyama Vingi vya Kiswahili Tanzania ni Suala Lenye Manufaa? Hili swali linapaswa kuulizwa kwa kila mdau wa Kiswahili vikiwemo vyombo vya kuratibu Kiswahili nchini Tanzania. Ni dhahiri kwamba kuna faida na hasara; lakini, je, upande upi ni mkubwa zaidi?

Machapisho kwa Lugha ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa nchini Tanzania, maandiko mengi yapo kwa lugha ya Kiingereza. Hata vitabu vingi vinavyojadili masuala ya Kiswahili vimeandikwa kwa Kiingereza. Karibia masuala mengine yote (kiasiasa, kiuchumi, kitamaduni, kijamii) yamendikiwa kwa lugha ya Kiingereza, hususan kama andiko ni la kitaaluma. Issaya Lupogo na Aziza Lupogo ni baadhi ya waandishi wachache ambao wameandika kitabu kinachotumika kama kitabu cha kiada katika Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda); kitabu hicho kina anwani: Nadharia ya Utofauti katika Ndoa na Mahusiano ya Kimapenzi. Dar es Salaam[1].

  1. Lupogo,I & Lupogo, A. (2019). Nadharia ya Utofauti katika Ndoa na Mahusiano ya Kimapenzi. Kiswahili Development Limited: Dar es salaam