Nenda kwa yaliyomo

Vyacheslav Volodin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vyacheslav Viktorovich Volodin (Kirusi: Вячеслав Викторович Володин; alizaliwa 4 Februari 1964) ni mwanasiasa wa Urusi ambaye anahudumu kama Mwenyekiti wa 10 wa State Duma (Bunge la Urusi) tangu mwaka 2016. Yeye ni msaidizi wa zamani wa Rais Vladimir Putin.

Akiwa Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha United Russia, alikuwa mbunge katika State Duma kuanzia mwaka 1999 hadi 2011 na tangu mwaka 2016 hadi sasa. Kuanzia mwaka 2010 hadi 2012, alikuwa Naibu Waziri Mkuu wa Urusi. Pia, aliwahi kuwa Naibu Mkuu wa Kwanza wa Utumishi wa Ofisi ya Rais wa Urusi (Kremlin).[1] Ana cheo cha juu cha utumishi wa umma cha serikali ya shirikisho kinachojulikana kama Mshauri Amilifu wa Serikali wa Daraja la Kwanza wa Shirikisho la Urusi.[2] Volodin ndiye aliyesimamia mabadiliko ya kihafidhina ya Putin katika muhula wake wa tatu na anahesabiwa kuwa miongoni mwa Watu wa karibu wa Putin.[3][4][5]

  1. Vyacheslav Volodin. themoscowtimes.com (accessed 14 October 2015)
  2. Kigezo:Cite act
  3. "Cluster bomb: How Russia is ruled". The Economist. 6 Aprili 2022. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2016.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Russia's Vladimir Putin Reshuffles Inner Circle". Courthouse News Service. 23 Septemba 2016.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Langton, James (15 Machi 2022). "Meet Russia's siloviki — Putin's inner circle". The National.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vyacheslav Volodin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.