Nenda kwa yaliyomo

Vusi Mahlasela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vusi Mahlasela akitumbuiza kwenye sherehe za miaka 100 ya kuzaliwa kwa Die Burger huko Cape Town, 2015.

Vusi Sidney Mahlasela Ka Zwane (alizaliwa mnamo 1965 [1]huko Pretoria, Afrika Kusini) ni mwimbaji maharufu na mtunzi wa nyimbo wa Kisotho nchini Afrika Kusini.

Muziki wake kwa ujumla hutambulika kama "African folk" na mara nyingi huitwa "The Voice" yani sauti ya Afrika Kusini. Kazi yake ilikuwa na msukumo kwa wengi katika harakati za kupinga ubaguzi wa rangi . Maudhui yake ni pamoja na mapambano ya uhuru, na msamaha na upatanisho na maadui. Vusi ametoa albamu saba za studio na alisainiwa na rekodi lebo ya Dave Matthews ATO Records mwaka 2003.

Vusi alitumbuiza wakati wa kuapishwa kwa Nelson Mandela mwaka 1994 na baadae alitumbuiza katika tafrija ya kuadhimisha kwa miaka 90 ya Nelson Mandela huko Hyde Park, London mwaka 2008, na katika Siku ya Mandela kwenye Ukumbi wa Muziki wa Radio City Julai 2009. Wimbo wake wa "When You Come Back" ulitumika kama wimbo wa ITV katika matangazo yao ya Kombe la Dunia mwaka 2010 [2] na Vusi alitumbuiza kwenye tamasha la FIFA la Kombe la Dunia katika Uwanja wa Orlando huko Soweto, Afrika Kusini. [3] Mnamo mwaka 2012, tuzo za SAMA (SAMA Awards) zilimtukuza Vusi na tuzo ya mafanikio ya maisha. [4]

  1. "BIO". VUSI MAHLASELA (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
  2. "When You Come Back (ITV World Cup theme version) – Vusi Mahlasela | Betting Island". 19 Agosti 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Agosti 2014. Iliwekwa mnamo 2020-03-20.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "FIFA WORLD CUP KICK–OFF CELEBRATION CONCERT | 10 June 2010 | Control Room". 10 Aprili 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Aprili 2010. Iliwekwa mnamo 2020-03-20.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "MTN SAMA 18 salutes Ray Phiri and Vusi Mahlasela - 18TH ANNUAL MTN SA MUSIC AWARDS". 14 Aprili 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Aprili 2012. Iliwekwa mnamo 2020-03-20.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vusi Mahlasela kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.