Nenda kwa yaliyomo

Vladimir Nabokov

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vladimir Nabokov 1973
Vladimir Nabokov
Faili:Vladimir Nabokov.jpg
Amezaliwa Vladimir Vladimirovich Nabokov
22 Aprili 1899
Saint Petersburg, Urusi
Amekufa 2 Julai 1977
Uswisi
Kazi yake Mwandishi, Profesa.
Ndoa Vera Nabokov
Watoto Dmitri Nabokov

Vladimir Nabokov (Kirusi Владимир Владимирович Набоков vladimir vladimirowich nabokov; 10 Aprili 1899 - 2 Julai 1977) alikuwa mwandishi kutoka nchini Urusi aliyekuwa baadaye raia wa Marekani.

Alizaliwa katika familia ya kikabaila akapata elimu nzuri akaaanza kutunga mashairi akiwa na umri mdogo na kutoa kitabu chake cha kwanza mwaka 1916.

Uhamisho wa Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Baada ya Mapinduzi ya Urusi ya 1917 familia ilikimbia na kuhamia Ulaya ya Kati na Magharibi. Vladimir alianza kusoma sayansi na fasihi kwenye chuo kikuu cha Cambridge (Uingereza). 1922 baada ya kifo cha baba alijiunga na familia iliyokuwa na nyumba mpya huko Berlin (Ujerumani). Hapa Vladimir alifanya kazi kama mwalimu wa nyumbani akaendelea kuandika na kutoa riwaya zake za kwanza. 1925 alimwoa Mrusi mwenzake Vera Jevseyevna Slonim akaendelea kuandika. Riwaya 9 alitoa wakati alipoishi Ujerumani.

Tangu 1933 hali ya familia ilikuwa vigumu baada ya chama cha Nazi kuchukua serikali ya Berlin kwa sababu mke wake Vera alikuwa Myahudi. 1934 mtoto wa pekee Dimitri alizaliwa. 1936 waliondoka Ujerumani wakakaa Ucheki na baadaye Ufaransa. Vladimir alianza kuandika kwa Kiingereza.

Marekani[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1940 wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia familia ilikimbia wakafaulu kupata nafasi kwenye meli kwenda Marekani iliyoondoka Ufaransa wakati jeshi la Ujerumani limeshaanza kuvamia nchi. Vladimir alipata kazi kama bingwa wa vipepeo kwenye American Museum of Natural History mjini New York kwa muda kidogo lakini aliendelea kuwa mwalimu wa fasihi kwenye vyuo mbalimbali na tangu 1948 profesa wa fasihi kwenye chuo kikuu cha Cornell. Tangu 1945 alikuwa raia wa Marekani.

1955 alitoa kitabu kilichoendelea kumfanya mtu maarufu kimataifa na kumpatia mapato makubwa. Riwaya "Lolita" ilisimulia habari za mapenzi kati ya mwanaume mzee na binti mdogo. Baada ya kufaulu vema kiuchumi aliacha kazi yake kwenye chuo kikuu na 1961 akahamia Montreux (Uswisi) pamoja na mke wake alipoaga dunia mwaka 1977.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vladimir Nabokov kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.