Vladimir Chub
Mandhari
Vladimir Fyodorovich Chub (alizaliwa 24 Julai 1948) ni mwanasiasa wa Urusi aliyekuwa Gavana wa Mkoa wa Rostov kuanzia mwaka 1991 hadi 2010. Aliteuliwa kuwa gavana mnamo Oktoba 1991 na baadaye mwaka huo alishinda uchaguzi wa nafasi hiyo kwa kura nyingi. Alichaguliwa tena mnamo mwaka 1996 na 2001. Aliteuliwa kujiunga na Baraza la Shirikisho (Federation Council) mnamo mwaka 1993.[1]
Kabla ya kuwa gavana, alikuwa Katibu wa Kwanza wa kamati ya chama cha CPSU katika wilaya ya Proletarian mjini Rostov.[2] Yeye ni mwanachama wa chama cha Urusi ya Pamoja (United Russia), na zamani alikuwa mwanachama wa vyama vya NDR, na OKS.[3] Serikali yake ilichukua msimamo mkali dhidi ya shughuli za kisiasa zilizo kinyume cha sheria. Chub ana asili ya Ukraine.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Russia Profile - Who's Who?". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-06. Iliwekwa mnamo 2006-02-15.
- ↑ "Persons - NUPI". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-02-24. Iliwekwa mnamo 2006-02-15.
- ↑ "Московский Центр Карнеги - Журнальный столик - Публикации сотрудников МЦК - United Russia: a Fast-build Party Structure for the Kremlin and the Governors". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-27. Iliwekwa mnamo 2006-02-15.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vladimir Chub kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |