Vitabu vya nyimbo za shule ya msingi (Kijapani)
Vitabu vya nyimbo za shule ya msingi (Kijapani: Shōgaku Shōka Shū) ni mfululizo wa vitabu vya nyimbo vilivyokusanywa kwa ajili ya elimu ya shule na Wizara ya Elimu ya Japani kupitia kamati ya utafiti ya muziki ,ambayo ilianzishwa mwaka 1879 na Isawa Shuji.Vitabu hivyo vya nyimbo vilichapishwa kuanzia mwaka 1881 hadi 1884 kwa jumla ya sehemu tatu. Mfululizo huu ulikua wa kwanza kutumia alama rasmi za muziki kwenye vitabu vya muziki wa Kijapani.
Sehemu ya kwanza ilikua na nyimbo 33, sehemu ya pili ilikua na nyimbo 16, na sehemu ya tatu ilikua na nyimbo 42. Nyimbo nyingi zilikua zinachimbuko la maandishi ya Kijapani lakini ziliimbwa kwa kutumia midundo ya magharibi zilizochukuliwa kutoka kwenye nyimbo kama Hänschen klein" katika sehemu ya kwanza, "Alle Vögel sind schon da" kwenye sehemu ya pili, na "The Last Rose of Summer" kama sehemu ya tatu.