Visiwa vya mfereji wa Kiingereza

Visiwa vya Mfereji wa Kiingereza ni funguvisiwa la visiwa tisa katika Mfereji wa Kiingereza karibu na pwani ya Ufaransa vyenye wakazi 160,000.
Visiwa vitano vikubwa ni:
Kiutawala vimegawiwa sehemu mbili: eneo la Jersey na eneo la Guernsey lakini visiwa kadhaa vina kiasi kikubwa cha uhuru peke yao.
Hali ya kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Visiwa hivi vina hali ya pekee. Vyote ni "maeneo chini ya taji la Uingereza" lakini si sehemu za Ufalme wa Muungano wala Uingereza wenyewe. Havishiriki katika bunge la London wala havipaswi kupokea sheria za bunge hili bali vina bunge zao za Jersey, Guernsey, Alderney na Sark pamoja na watendaji na mahakama. Mfalme wa Uingereza ana wajibu wa kutetea visiwa na kushughulika mambo ya nje. Hali halisi wajibu huo unangaliwa na serikali ya Uingereza kwa niaba ya mfalme. Mwakilishi wa mfalme yaani serikali ya Uingereza ni Gavana.
Madaraka ya mfalme) yametokana na cheo chake cha kale kama Mtemi Mkuu wa Normandy miaka 800 iliyopita. Kihistoria visiwa vilikuwa sehemu ya Normandy na mwaka 1066 mtemi wa Normandy alishambulia na kuteka Uingereza. Kuanzia hapo waandamizi wake wameendelea na vyeo viwili vya Mfalme wa Uingereza na Mtemi wa Normandy na hivyo mkuu wa visiwa. Katika karne iliyofuata wafalme wa Ufaransa walitwaa Normandy lakini walishindwa kuteka visiwa vidogo. Hali ya visiwa haikubadilishwa kisheria: havikuunganishwa na ufalme wa Uingereza, hivyo hadi leo ni mabaki madogo ya mali ya wafalme wa Uingereza katika Ufaransa wa leo.
Utamaduni
[hariri | hariri chanzo]Watu wengi huzungumza Kiingereza; hata hivyo wengine huendelea kuongea lugha zao za asili ambazo ni aina za Kinormandy kinachozungumzwa pia kama lugha ya kieneo Ufaransa bara. Idadi ya wasemaji imepungua kuna hasa maelfu kadhaa Guernsey na Jersey. Lugha rasmi kwa shughuli za serikali ni hasa Kiingereza lakini pia Kifaransa.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi wa visiwa umetegemea hasa utalii, huduma za benki na kilimo.
Kwa kuwa visiwa hivyo si sehemu za Uingereza wala za Umoja wa Ulaya viko ndani ya ushuru wa pamoja wa Ulaya lakini vina haki ya kuongeza kodi zao.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya mfereji wa Kiingereza kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |